Mbwana Sammata ndio mchezaji mwenye profile kubwa zaidi kwa upande wa wachezaji wetu wa timu ya taifa. Amepita kwenye klabu kubwa tofauti tofauti na kuonesha uwezo wa kuvutia.
Mechi ya Simba dhidi ya TP Mazembe ndio ilimpa dili kujiunga na miamba hiyo ya DRC. Alifunga goli moja la kichwa licha ya Simba Sc kupoteza mechi kwa magoli 3-2 lakini yeye binafsi alikua na mchezo mzuri sana.
Tp Mazembe ilimfanya aonekane zaidi kutokana na ubora wa timu hiyo pamoja na performance yake kubwa. Kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani ya Africa sio kitu kidogo.
Pale Genk alifanya mabalaa sana mpaka wazungu wakamtungia nyimbo ni miguu yake na kichwa chake kilifanya aimbwe.
Akatua Aston Villa hakudumu sana lakini alitimiza ndoto za kucheza moja ya ligi ngumu na kubwa duniani. Aliwafunga Liverpool kamba ya viwango,ile ndoo aliyopiga unanikumbuka?
Maisha yakampeleka Fernebache mambo hayakua mazuri sana kwake. Akarudi nyumbani (Genk) akatwanga kwa muda halafu akajiunga na timu nyingine ya hapo hapo Belgium
Royal Antwerp napo hakukaa sana na mpaka kuelekea AFCON hii yupo na miamba ya Ugiriki PAOK. Huyu ndio Mbwana Sammata 'Popa'