Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndiye Diarra anayewahakikishia ulinzi na usalama Wananchi wa Jangwani

Diarra Tizii Huyu ndiye Diarra anayewahakikishia ulinzi na usalama Wananchi wa Jangwani

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sio kwa bahati mbaya yeye kumuweka nje Mlinda lango anayecheza Ulaya katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Mali.

Uwezo wake ni mkubwa sana ukilinganisha na walinda lango wengne, anaweza asiwazidi katika ball catching au mipira ya krosi ila kuna sifa anazo ambazo wengine wana 20% wakati yeye ana 99%.

✅Leadership Skills or Qualities Diarra uwezo wake wa kuongea na kuwapanga walinzi wake ni wa kiwango cha hali ya juu. Golikipa ananafasi kubwa ya kuuona mchezo kama sisi watu wa nje kwa maana yeye ndiye anawaona wachezaji wake na sura nzima ya mchezo.

Pale mchezaji anapokosea Diarra sio tu humfokea bali hutoa maelekezo kabisa kuwa unatakiwa kukaa sehemu hii kama mpira utakua sehemu fulani, unatakiwa kuwa sehemu hii kama mpira utakuwa pale.

Huu ndo upeo aliopewa huyu nyanda kutoka Mali, lakin anaongea mnoo na ni mwepesi ku-react kwenye matukio kadhaa. Kuna nafasi kama mbili alizipata Wamba mshambuliaji wa Belouzdad lakini wepesi wa Diarra kutoka kulipunguza lango uliendelea kuiweka yanga salama.

✅Ball Playing Hii nadhani haina ubishi uyo ndo doctor na mwalimu wa Walinda milango likija suala zima la kuuchezea mpira, Belouzdad walianza kwa kupress dakika za mwanzo wakidhani golikipa ni yule yule waliyekutana naye Algeria lakini baada ya dakika kadhaa wakaona wanapoteza muda wao bure wakaamua kurudi nyuma.

Hii ndiyo sifa ya Diarra, ukija kichwa kichwa anakunyoosha na pressing zako na unaenda kusimulia.

✅Motivation Speaker Hii nayo ni sifa ya Diarra, akiamua kuhamisha jambo basi kila mtu ataelewa, kama mnatafta bao basi atawafanya muone kazi ni nyepesi kwa maneno yake au ishara zake.

Lakin pia huwa anatoa ushauri mzuri kwa mtu kama kafanya mistake kisha kumfanya aone anaweza kurekebisha makosa yake.

✅Analeta Utulivu kwenye safu ya Ulinzi Nadhani hii haiitaji maelezo mengi, kuna tofauti Yanga Sc ikicheza na Diarra na ikicheza na walinzi wengine langoni. Diarra Djigui, Malian Soldier made from Stade Malien.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live