Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio mbaya wa Samatta PAOK

Samatta X Brandon Huyu ndio mbaya wa Samatta PAOK

Sun, 27 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Mbwana Samatta, PAOK Thessaloniki imeanza kibabe msimu huu ambapo haijapoteza mechi zote sita za mashindano tofauti ilizocheza hadi sasa, lakini nahodha huyo wa Taifa Stars bado hajapata muda mwingi wa kucheza chini ya kocha Razvan Lucescu, raia wa Romania.

Katika mechi hizo ambazo PAOK imeshinda nne na kutoka sare mbili, Samatta amecheza michezo mitano, huku minne akitokea benchi na mmoja akianza kikosini, lakini imeonekana mshambuliaji raia wa Hispania, Brandon Thomas ndiye amekuwa kikwazo kwa nyota huyo kupata nafasi ya kucheza.

Brandon (28) aliyejiunga na PAOK mwaka jana akitokea Malaga ndiye amekuwa akianzishwa na pia kupishana na Samatta pale timu hiyo inapofanya mabadiliko katika idadi kubwa ya mechi.

Mchezo wa mwisho ni wa juzi ugenini wa Mashindano ya Europa Conference League ambao PAOK iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ulioshuhudiwa Brendan Thomas akianza na kucheza kwa dakika 88 huku Samatta akishindwa kuwepo hata benchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live