Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio Sadio Kanoute (Putin), Injini haswa pale Simba

Kanoute Aucho Sadio Kanoute

Sat, 15 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sadio kiasili si kiungo ambae role yake ni kubaki chini muda mwingi kwa maana ya holding midfielder, defensive midfielder au deep lying playmaker, Sadio ni box to box midfielder, ni mzuri kama utahitaji abadilike kutoka na vipindi ndani ya uwanja, acheze baina ya maboksi mawili, alinde timu yake isipokuwa na mpira na ashambulie timu yake ikiwa na mpira.

Pale Simba anacheza pacha na Mzamiru Yassin ambae pia ni mzuri akicheza kama box to box, Sadio analazimika kubaki chini zaidi ingawa kiasili yeye ni kiungo wa kutembea zaidi, jambo zuri anatekeleza kwa ufasaha majukumu ambayo si ya asili yake, yani ni sawa na mwalimu ambae ni mtaalamu wa kuchora akafundishe mziki ambao si asili yake, kwa bahati nzuri akatendea haki majukumu hayo.

Udhaifu wa Sadio ni kukosa umakini wa pasi katika baadhi ya nyakati, anaweza kupoteza pasi rahisi ambayo hukuitegemea kupoteza, ingawa mazuri yake ni hatari aliyonayo kama akilikaribia box, anapiga sana, anajua sana kuzishambulia second balls ( mipira ya pili ), anaruka sana vichwa, nafikiri kwa wachezaji wa Simba anaweza kuwepo kwenye top three ya wachezaji wao ambao ni hatari kwenye mipira ya juu

Sadio ni mchezaji mwenye fiziki sana, anaweza kucheza kwa spidi ileile katika dakika zote tisini, anafika sana kwenye mpira kwa sababu ya uwezo wake mkubwa katika kuzuia, anagongana sana, na pia yupo tayari kucheza faulo ya aina yeyote ambayo itakuwa ni chachu kwa timu yake kubaki salama, maana halisi ya kiungo mkabaji, maana halisi ya mpambanaji ndani ya timu.

Imeandikwa na Salehe Mawele

Chanzo: www.tanzaniaweb.live