Wataalamu wa uchambuzi wa data katika soka wamekusanya data na kufanya hesabu kuona ni timu gani msimu wa 2023-24 ina nafasi kubwa ya kutwaa taji la Premier League (Ligi Kuu ya Uingereza).
Katika uchambuzi huo wa data, viwango vya wachezaji vitapimwa namna makocha ambavyo wataongoza timu hizo na uelewa wa mchezo kwa ujumla.
1. MANCHESTER CITY – 90%
Msimu wa 2022-23, Man City walitwaa mataji matatu, hivyo bado wanatarajiwa kutawala ndani ya Premier League.
City wamekuwa na kikosi chenye wachezaji bora wenye viwango vya juu, kwa msimu huu wana asilimia 90 za kutwaa taji la ligi.
2. ARSENAL – 4%
Msimu uliopita Arsenal walikaa kileleni mwa msimamo wa Premier kwa siku 248, iliwashangaza wengi kuona mwisho wa siku wamekosa ubingwa uliobebwa na Man City.
Safari hii mambo yanaweza kuwa tofauti, wanatakiwa kujipanga na kuwa na hesabu nzuri tofuti na msimu uliopita.
Hapa wamepewa asilimia nne tu za kutwaa ubingwa na kung’oa utawala wa Man City.
3. LIVERPOOL – 4%
Katika kipindi hiki cha majira ya joto wamefanya usajili makini ambao ni wazi utaimarisha timu hiyo japo bado wanahitaji kufanya kitu kabla ya dirisha kufungwa.
Hapa Opta amewapa Liverpool asilimia nne za kutwaa Premier League msimu huu.
Katika msimu wa 2022-23, Liverpool hawakuwa katika ubora wao ingawa mwanzo walionekana kuwa angeweza kushindana na Man City.
4. MANCHESTER UNITED – 2%
Ni kama wamefanya usajili mzuri japo hawajacheza kwa kiwango bora katika mechi zao mbili za awali msimu huu.
Man United wamefanikiwa kumsajili kipa Andre Onana na kiungo Mason Mount. Wakasajili straika kijana Rasmus Hojlund. Kwa namna mambo yalivyo, Opta amewapa United asilimia 2 kutwaa taji la Premier League.
5. NEWCASTLE UNITED – <1%
Wameonekana kujiimarisha tagu kuanzia msimu uliopita ikiwa ni moja ya timu bora ndani ya Premier League, hii ni baada ya kuuzwa kwa Waarabu wa Saudi Arabia, Oktoba 2021.
Ubora waliouonesha msimu uliopita, umeifanya Newcastle kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu baada ya kumaliza ndani ya top 4 katika Premier League. Hapa wamepewa nafasi ndogo ya kutwaa Premier.