Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu hapa mwanaume alioharibu shughuli ya Yanga

Huyu Hapa Mwanaume Alioharibu Shughuli Ya Yanga Huyu hapa mwanaume alioharibu shughuli ya Yanga

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ingizo la Adolf Mtesigwa kwenye kikosi cha Azam katika eneo la kiungo wa ulinzi kuliifanya timu kuwa imara zaidi kwa sababu ni mchezaji ambaye alikuwa hatoki kwenye eneo lake.

Kwa hiyo kila wakati ambapo Aziz Ki alikuwa akitaka kutumia eneo hilo alikuwa anakutana na Mtesigwa, ikamuondolea uhuru Aziz Ki.

Mbali na Zayd kuwa bora kwenye eneo la katikati ya uwanja lakini kimbinu Mtesigwa ndio alikuwa anatia ugumu kwa Yanga.

Viungo wengine wa Azam kama Akaminko na Bajana wakati timu yao inashambulia huwa wanapanda kusaidia mashambulizi na kuacha maeneo yao yakiwa wazi.

Jana Mtesigwa alikuwa hatoki kusogea juu hata wakati Azam inashambulia, kwa hiyo ikitokea mchezaji wa Yanga kapokea mpira mbele ya mabeki wa Azam, Mtesigwa anakuwa wa kwanza kuziba nafasi.

Wachezaji wa Yanga wakawa wanalazimika kupitia pembeni na sio katikati kwa Aziz Ki ambaye ndio huwa mtu hatari zaidi kupiga pasi za mwisho au kufunga.

Uchambuzi huo umetolewa na mkongwe Amri Kiemba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live