Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu hapa mrithi wa Van Dijk Liverpool

Liverpool Centre Back Virgil Van Dijk Sportingpcp Centre Back Goncalo Inacio Huyu hapa mrithi wa Van Dijk Liverpool

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa ripoti, Liverpool imeanza mazungumzo na Sporting Lisbon na Ureno kwa ajili ya kuipata saini ya beki kisiki wa timu hiyo na Ureno, Goncalo Inacio, 22, katika dirisha hili kama mbadala wa Virgil van Dijk.

Liverpool inaamini hata kama Van Dijk atasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, hatokuwa na muda mrefu sana wa kuwatumikia kutokana na umri wake, hivyo wanataka kuanzisha kizazi kipya kitakachowapa uhakika wa kupata huduma kwa muda mrefu.

Inacio ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha michuano ya Euro iliyofanyika Ujerumani mwaka huu, katika mkataba wake unaomalizika 2027, kuna kipengele kinachomwezesha kujiunga na timu yoyote ikiwa italipa Euro 60 milioni.

Inacio alionyesha kiwango bora katika kikosi cha Lisbon msimu uliopita ambapo alicheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao manne, amekuwa akihusishwa pia na Manchester United ambayo inapambana kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota huyo ametajwa pia katika timu mbalimbali Ulaya ambao zimekuwa zikimtolewa macho.

Hata hivyo ishu yaVan Dijk kwa upande mwingine imekuwa ikihusishwa na kuondoka kwa kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp aliyeamua kusepa na kupumzika kwa muda.

Vyovyote iwavyo, nahodha huyo wa Uholanzi atakapowekwa sokani timu nyingine huenda zikaibuka.

Wakati huo huo, mabosi wa Manchester City wamepanga kufanya mazungumzo na mshambuliaji kutoka Argentina, Julian Alvarez, 24, wiki hii baada ya kumaliza kuitumikia Argentina kwenye Copa America ambako walichukua ubingwa mbele ya Colombia.Timu kibao zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyo ikiwa ni pamoja na PSG inayomwangalia kama mbadala wa Kylian Mbappe aliyetua Real Madrid.

BEKI wa Arsenal na Poland, Jakub Kiwior, 24, ameambiwa kwamba ataruhusiwa kuondoka katika dirisha hili la usajili Ulaya ikiwa kuna timu yoyote kati ya zile zinazohusishwa kumhitaji itawasilisha ofa mezani. Staa huyu ambaye hakufanya vizuri katika michuano ya Euro mwaka huu akiwa na Poland amekuwa akiwindwa na timu kibao kutoka Serie A.

JUVENTUS ipo katika hatua za nzuri kuipata saini ya kiungo wa Atalanta na Uholanzi, Teun Koopmeiners, 26, ambaye pia anawindwa na timu ya Liverpool inayohitaji huduma yake katika dirisha hili la usajili. Teun ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027 katika msimu uliopita alicheza mechi 51 za michuano yote Ulaya.

KOCHA wa Barcelona, Hans Flick amemweka winga wa Athletic Bilbao, Nico Williams katika orodha ya juu ya wachezaji anaohitaji wasajliwe katika dirisha hili. Taarifa kutoka Hispania zinaeleza, Barca itakutana na wawakilishi wa staa huyo wiki hii kwa ajili ya mazungumzo zaidi. Rais wa La Liga, Javier Tebas wiki iliyopita alisema Barca inaweza kumsajili nyota huyo.

KIUNGO wa AS Monaco, Youssouf Fofana amewaambia mabosi wa timu hiyo kwamba anataka kuondoka kwenda kujiunga na AC Milan katika dirisha hili la usajili la majira ya joto linaloendelea duniani. Staa huyo amekuwa akihusishwa na timu nyingi barani Ulaya na hivi karibuni Monaco ilikataa ofa ya Euro 30 milioni kutoka kwa Nottingham Forest iliyoanza mapema kumfukuzia.

Inaelezwa staa huyo pia ameshafanya makubaliano na AC Milan lakini changamoto kubwa ipo kwa Monaco inayohitaji zaidi ya Euro 40 milioni ili kumwachia.

TRABZONSPORr ya Uturuki imeendelea kufanya mazungumzo na Liverpool kwa ajili ya kuipata saini ya beki wa timu hiyo Trabzonspor ya Uturuki katika dirisha hili baada ya ofa yao ya kwanza ya Pauni 4 milioni kukataliwa. Kwa mujibu wa taarifa mabosi wa Liverpool wapo tayari kumwachia lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 8 milioni. Mkataba unaisha 2025.

KIUNGO wa Crystal Palace, Adam Wharton, 20, ambaye anahusishwa na timu za Manchester City, Bayern Munich na Real Madrid amewaambia watu wake wa karibu kwamba hana mpango wa kuondoka Crystal Palace kwa sasa na badala yake anataka kucheza walau kwa msimu mmoja au zaidi ili kujiimarisha zaidi kabla ya kuamua hatima yake nyingine.

Adam ambaye mkataba wake unamalizika 2029. Msimu uliopita alicheza mechi 45 za michuano yote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live