Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu hapa kigogo anayetajwa United, ana balaa

Tajiri Huyu hapa kigogo anayetajwa United, ana balaa

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United ipo kwenye mchakato wa kumuajiri Dan Ashworth akawe mkurugenzi mpya wa michezo katika timu hiyo ambayo ina historia na rekodi za kipekee Englanda.

Ashworth ambaye kwa sasa anahudumu kwenye kikosi cha Newcastke United anadaiwa kuwa mmoja kati ya watu waliofanya mambo makubwa kwenye baadhi ya timu za Ligi Kuu England (EPL).

Akiwa na Brighton aliiwezesha kusajili mastaa wengi kwa pesa kiduchu kisha wakauzwa kwa mkwanja wa maana walipoondoka.

Hapa tunakuletea mastaa watano bora waliowahi kusajiliwa na mkali huyo wakati wa uongozi wake kwenye timu mbalimbali Ulaya.

Alexis Mac Allister

Licha ya safari yake ya mafanikio kuanzia West Bromwich alifanya makubwa akiwa na Brighton. Huko alisifika kwa uwezo wake mkubwa wa kutambua vipaji kutoka nchi zilizo nje ya Ulaya.

Mac Alliter alikuwa na umri wa miaka 20 wakati anasajiliwa na Brighton 2019 akitokea Boca Juniors. Brighton ililipa Pauni 650,000 kwa ajili ya kumnunua. Baada ya hapo ikaenda kumuuza kwa kiasi kisichopungua Euro 42 milioni.

Moises Caicedo Kwa mujibu wa gazeti la The Athletic, Ashworth alifanya kazi kubwa kuhakikisha staa huyo anatua Brighton.

Caicedo alisajiliwa kwa Pauni 4.5 milioni akitokea Independiente del Valle ya Ecuador, Februari 2021 na akauzwa kwa Pauni 115 milioni kwenda Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana. Chini ya Ashworth, Brighton ilikuwa na tabia ya kusajili wachezaji bora kwa pesa kiduchu kisha ikawauzwa kwa kiasi kikubwa.

Kaoru Mitoma

Ukiwaondoa Leandro Trossard na Marc Cucurella, Mitoma ni moja kati ya alama kubwa zilizowahi kuachwa na Ashworth kwenye kikosi cha Brighton. Staa huyo amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Kubwa zaidi ni kwamba alisajiliwa kwa kiasi cha Pauni 2.7 milioni mwaka 2021 akitokea Kawasaki Frontale.

Baada ya kusajiliwa Mitoma alitolewa kwa mkopo Royal Union Saint-Gilloise ya Ubelgiji kisha akarudi kuitumikia Brighton chini ya Graham Potter. Hadi sasa amecheza mechi 66, akifunga mabao 13 na asisti 14. Katika siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali kubwa za Ulaya.

Nick Pope

Alipojiunga na Newcastle United 2022, mtaalamu huyo alikuwa na nguvu kubwa ya kusajili mastaa kwa pesa kubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

Hii ilitokana na kiasi kikubwa cha uwekezaji ambacho kiliwekwa mezani na wamiliki wapya wa timu hiyo. Akafanikiwa kumsajili Pope aliyejiunga kwa Pauni 10 milioni akitokea Burnley.

Alexander Isak

Pauni 60 milioni ndizo pesa nyingi zaidi zilizowahi kutumiwa na Ashworth kwenye kusajili wa mchezaji. Akiwa bosi wa Newcastle aliidhinisha kiasi hicho cha fedha ili kumsajili Isak.

Inaelezwa kwamba Ashworth alifanya majadiliano ya muda wa siku mbili kabla ya kufikia makubaliano ya kutoa kiasi hicho cha pesa ambacho kwa kiasi chake kimeokana kuanza kuzaa matunda.

Hadi sasa Isak amefunga mabao 24 katika mechi 52 za michuano yote alizocheza Newcastle United.

Chanzo: Mwanaspoti