Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu asiyejulikana ndani ya Yanga ni nani?

Yanga Ngao Ya Jamii 2023 24 Tt Huyu asiyejulikana ndani ya Yanga ni nani?

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pengine kwa miaka ya 2000's basi Klabu ya Yanga ya misimu hii mitatu ndio hatari zaidi uthibitisho wa namba unafanya wazo hili kua fact.

Misimu miwili nyuma ilikua bingwa wa Vikombe vingi vya ndani na medali ya CAF Ngazi ya Shirikisho, Hii haijawahi kutokea kwenye historia yao.

Ukimuuliza kila Mwananchama, Shabiki, Viongozi au mdau yeyote wa soka atakwambia ubora wa Yanga miaka miwili nyuma ilikua Kocha Nabi na Fiston Mayele.

Hao wangeanza alafu yangekuja maelezo mengine yakujazia karatasi ili kukusanya Insha ya Wasifu yenye kueleweka.

Aliyekua Mkurugenzi wa ufundi wa Bayern Munich Hassan Salihamidzic aliwahi kusema Kazi ngumu kuunda timu, Kazi ngumu zaidi kuibakisha timu inapoharibika.

Huyu baada ya kuondoka Lewandowski alishindwa kupata tiba na Bayern ikawa nyonge Ulaya na ndani, mpaka Hassan akapoteza kazi yake.

Yanga walipopoteza Wachezaji wengi bora machoni mwetu Fiston Mayele, Djuma Shaban na Bangala mbaya zaidi Kocha Mkuu na wa viungo wengi waliamini Mwisho wa Zama zao

Hata kwenye usajili wao hawakuonekana kutisha sana, Lakini HAPA NI WAPI !? Timu imekua bora mara dufu, Ramani ya Nabi imemsaidia vema Gamondi.

Ameibadolisha timu muda mfupi, Hakuna anayehitaji kukutana na Yanga wakati huu, Upande wa pili Wachezaji waliosajili 80% Wamekua bora na kusahau waliopita.

Kuna mtu anastahili pongezi hizi mbaya tu hatujui nani mwenye hili jicho la kitaalamu mpaka kufika hapa, Rais wa klabu naamini anasimamia Malipo na saini tu.

Kuna Kichwa nyuma ya Ramani hii ni nani? Ameifanya kazi ambayo wengi wameshindwa ikiwemo Bayern Munich, Hata Barcelona iliwashinda.

Hawajawahi kutangaza Mkurugenzi wa ufundi wala Skauti wa kushughulikia hiki kinachoendelea kwao. Mwenye kumjua amtaje na ampe maua yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: