Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu Ngoma kama Mkude tu - Oscar Oscar

Ngoma Mkude0004 Huyu Ngoma kama Mkude tu - Oscar Oscar

Thu, 28 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sasa mashabiki wa Simba wako katika kilele cha furaha kutokana na kiwango ambacho kinaonyeshwa na Kiungo Mkongomani Fabrice Ngoma tangu atue hapo Unyamani.

Fabrice Luamba Ngoma ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu,pasi fupi fupi na zikafika kwa wahusika kitu ambacho anawashinda kina Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Kutokana na ubora wa Kiungo huyo ikabidi nirudishe kumbukumbu zangu nyuma nikaona kwamba sifa za Fabrice Ngoma pia anazo Kiungo wa zamani wa Simba Jonas Mkude ambaye kwa sasa yupo Yanga.

Wakati ule wa miaka 4 ya utawala wa Simba kwenye soka letu hiki ambacho anakifanya Fabrce Ngoma ndio kile ambacho kilifanywa pia na Jonas Mkude kwenye uzi mwekundu na mweusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live