Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu Diarra anatisha nyie!

Diarra Pic Data Screen Protector Djigui Diarra

Sun, 27 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kiwango bora kilichoonyeshwa na kipa Djigui Diarra katika raundi zilizopita za Ligi Kuu Bara kimewaibua mastaa mbalimbali wakimzungumzia na kuelezea jinsi walivyoshindwa kumtungua kipa huyo raia wa Mali anayekipiga Yanga.

Diarra umekuwa mwiba kwa washambuliaji kwani hadi hivi sasa ameruhusu mabao manne tu langoni mwake huku akiwa na ‘clean sheet’ 10 katika michezo 14 aliyocheza huku akifuatiwa na Aishi Manula wa Simba mwenye tisa.

Straika wa KMC, Matteo Anthony ni miongoni mwa washambuliaji waliobaniwa kutikisa nyavu na Diarra kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ambao KMC alipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 wakiwa ugenini ambapo alisema;

“Sikutegemea kama ule mpira angeweza kuudaka kwani kabla sijapiga nilishaangalia wapi nipige huku nikidhani anaweza kwenda upande mwingine lakini haikua hivo kutoka na ubora wake alionao na jinsi alivyokuwa makini langoni,” alisema Matteo na kuongeza;

“Hadi hivi sasa yeye ndiye golikipa hatari zaidi nampongeza na wala siwezi kuficha hilo kutokana na takwimu zake hivyo nategemea mwisho mwa msimu kuona akipata mafanikio zaidi na kitu cha msingi ni kwamba atakua fundisho kwa magoli kipa wengine.”

Naye straika wa Geita Gold, George Mpole alisema kuwa licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga katika mchezo wao dhidi ya Yanga kule mkoani Mwanza bado lile bao alilokosa mbele ya Diarra linampa maswalim mengi ingawa sababu kubwa ya kilichotokea ni uhodari wa kipa huyo.

“Naweza kusema Diarra alikaa sehemu sahihi na umakini wake ulikuwa wa kipekee sana kwani ni mara chache makipa kuokoa mabao ya namna hile na hichi ndicho kinamfanya haonekane bora zaidi msimu huu lakini kwa upande nilipiga vyema tena bila wasiwasi lakini haikua bahati yangu kuwafunga Yanga.”

Aidha Atupele Green wa Biashara United alisema;”Diarra sio kipa wa kubeza kwani ubora wake unadhijirisha umairi wake na ukubwa na ndio maana aliungana na timu yake ya taifa ya Mali hivyo sio goli kipa wa kitoto, kwangu nadhani yeye ndiye goli kipa bora msimu huu.”

“Na pia kuna mengi amekuja kuwafunza makipa wengine wa ligi yetu lakini watakao nufaika zaidi ni wale wanaocheza naye timu moja kwani wanafanya mazoezi pamoja licha hivyo mimi nampa pongezi kubwa kwa kiwango chake,” alisisitiza Atupele.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz