Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huwa nawaambia vijana wangu wacheze kama tunafanya mazoezi - Gamondi

Pacome Gamondi Maxi Huwa nawaambia vijana wangu wacheze kama tunafanya mazoezi - Gamondi

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa huwa anawaambia wachezaji wake kwenye mechi wacheze kama wanavyofanya mazoezi tu.

Gamondi amesema hayo jana baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Ihefu FC ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 5-0 na kuifanya kuwa Timu ya nane kupokea dozi ya bao tano kutoka kwa Yanga msimu huu.

Gamondi ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo waliyoyapata timu yake dhidi ya Ihefu Sc licha ya mchezo huo kuonekana ulikuwa mgumu kwao huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kufuata maelekezo yake.

"Tumecheza vizuri sana, tuliwaheshimu Ihefu wamecheza vizuri na walijitahidi kumiliki mpira. Tulitengeneza nafasi nyingi na kuzitumia baadhi.

"Kipindi cha kwanza Ihefu ilicheza na watu wengi kwenye eneo lake la ulinzi lakini tulikuwa na mbinu nzuri na tulifanyia kazi hilo kulitafutia ufumbuzi.

"Kipindi cha pili Ihefu walikuja kwa nguvu ili kutaka kupata magoli, tukafanya mabadiliko ya kimbinu kwa kumuingiza Guede na Okrah ili kutumia speed yake [Okrah] kwenye mashambulizi ya kushtukiza ‘counter attacks’ na ilitulipa.

"Mara zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu tucheze kama tulivyofanya mazoezi na tumeonesha kile ambacho tulikuwa tukikifanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi," amesema Miguel Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: