Kuna double standard fulani hivi tumezitengeneza kwenye Klabu za Simba na Yanga, nadhani hii pia inaanzia katika maeneo mbalimbali kwa namna ambavyo wanachukuliwa.
Mbaya zaidi imeanza kuingia hadi kwa mashabiki kuna ukubwa fulani hivi wamejiwekea ambao haupo katika taratibu za kimpira.
Hakuna sehemu yoyote ambayo imeandikwa au ipo kuwa Simba na Yanga hawapaswi kuzidiwa kimchezo wala kufungwa.
Dakika za mwisho mashabiki walirusha mawe uwanjani kuashiria kutopendezwa na mbinu za mchezo ambazo kwa timu yoyote ile ambayo imeshinda lazima ingefanya tu ambacho ni kupoteza muda.
Too bad kama wenye maamuzi kwa maana ya bodi ya ligi kwa haraka watashindwa kumalizana na Yanga mapema huenda ikawa saratani kubwa huko mbeleni.