Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Huu ni msimu wangu wa mwisho Liverpool' - Mo Salah

'Huu Ni Msimu Wangu Wa Mwisho Liverpool'   Mo Salah.png 'Huu ni msimu wangu wa mwisho Liverpool' - Mo Salah

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: Bbc

Mohamed Salah anasema ni "mwaka wake wa mwisho" ndani ya Liverpool na kwamba hakuna mtu katika klabu hiyo ambaye amezungumza naye kuhusu mkataba mpya.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake wa sasa huko Anfield unatarajiwa kuisha msimu ujao, alifunga bao katika ushindi wa 3-0 wa The Reds dhidi ya Manchester United Jumapili.

Salah alisema baadaye alichukulia mechi hiyo kana kwamba ilikuwa ya mwisho kwake Old Trafford.

"Nilikuwa naingia kwenye mchezo, nilikuwa nikisema, 'angalia, inaweza kuwa mara ya mwisho'," aliiambia Sky Sports.

"Hakuna mtu katika klabu ambaye alizungumza nami kuhusu mikataba kwa hivyo nilikuwa kama, 'Sawa, ninacheza msimu wangu wa mwisho na kuona kitakachofanyika mwisho'.

"Ninahisi niko huru kucheza soka, tutaona kitakachotokea mwaka ujao." Alipoulizwa kuhusu maoni ya Salah, meneja Arne Slot alisema: "Tuna ‘pengine’ nyingi. Kwa sasa yeye ni mmoja wetu na ninafurahi sana yeye kuwa mmoja wetu na alicheza vizuri sana.

"Sizungumzii kuhusu mikataba kutoka kwa wachezaji lakini ninaweza kuzungumza kwa saa nyingi jinsi Mo alivyocheza leo."

Mwezi Julai 2022, Salah alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu, na kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, akilipwa zaidi ya £350,000 kwa wiki.

Chanzo: Bbc