Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu ndiyo uchungu wa mama kwa Kibabage

Kibabage Ushindi Goli Huu ndiyo uchungu wa mama kwa Kibabage

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mama mzazi wa beki wa Yanga, Nickson Kibabage, Flora Ngwido ameitaja mechi iliyowahi kumuumiza zaidi wakati mwanaye akiwa ndani ya kikosi hicho.

Kibabage ambaye ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri alisajiliwa msimu huu akitokea Singida Fountain Gate aliyoichezea kwa miezi sita kabla ya kwenda Yanga, ambako anacheza nafasi moja na Mkongomani Joyce Lomalisa.

Akizungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake mjini Morogoro, Flora amesema mtoto wake anapokuwa uwanjani siyo nyakati zote huwa ni nzuri kwake na kama mzazi yapo mengi yaliyowahi kumuumiza.

Amesema jambo linalomuumiza zaidi ni kumuona Kibabage anaanguka au kupata majeraha akieleza kuwa tukio hilo likitokea kama mama hushindwa kuendelea na kuangalia mpira.

"Yanga walipokuwa ugenini dhidi Medeama (Ghana) katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika niliumia sana kwani Kibabage alifunga bao na wamuzi akasema ni offside (ameotea) wakati ni goli.

"Ile mechi kuna muda aliangushwa chini nikasema basi tena hatainuka. Nikaamua kuondoka kabisa nisiendelee kuitazama ila baada ya muda nikaitwa kuambiwa anaendelea kucheza,"anasema mzazi huyo.

Anaongeza kuwa, "kiukweli kikimtokea kitu chochote cha kumuumiza natamani atoke apumzike kwanza kwani moyo unashindwa kabisa kuvumilia shida yoyote anayopata."Huu ndiyo uchungu wa mama kwa Kibabage

VICTORIA MELKIAD

Mama mzazi wa beki wa Yanga, Nickson Kibabage, Flora Ngwido ameitaja mechi iliyowahi kumuumiza zaidi wakati mwanaye akiwa ndani ya kikosi hicho.

Kibabage ambaye ni miongoni mwa wazawa wanaofanya vizuri alisajiliwa msimu huu akitokea Singida Fountain Gate aliyoichezea kwa miezi sita kabla ya kwenda Yanga, ambako anacheza nafasi moja na Mkongomani Joyce Lomalisa.

Akizungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake mjini Morogoro, Flora amesema mtoto wake anapokuwa uwanjani siyo nyakati zote huwa ni nzuri kwake na kama mzazi yapo mengi yaliyowahi kumuumiza.

Amesema jambo linalomuumiza zaidi ni kumuona Kibabage anaanguka au kupata majeraha akieleza kuwa tukio hilo likitokea kama mama hushindwa kuendelea na kuangalia mpira.

"Yanga walipokuwa ugenini dhidi Medeama (Ghana) katika mechi ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika niliumia sana kwani Kibabage alifunga bao na wamuzi akasema ni offside (ameotea) wakati ni goli.

"Ile mechi kuna muda aliangushwa chini nikasema basi tena hatainuka. Nikaamua kuondoka kabisa nisiendelee kuitazama ila baada ya muda nikaitwa kuambiwa anaendelea kucheza,"anasema mzazi huyo.

Anaongeza kuwa, "kiukweli kikimtokea kitu chochote cha kumuumiza natamani atoke apumzike kwanza kwani moyo unashindwa kabisa kuvumilia shida yoyote anayopata."

Chanzo: Mwanaspoti