Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu hapa uzi mpya Azam FC 2024/25

Azam FC Jersey 2024 25 Huu hapa uzi mpya Azam FC 2024/25

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Dar, Azam FC wamezindua uzi mpya kwa ajili ya msimu wa 2024/25 ambao ni bora kwelikweli ukiwa ni mtoko wa Dunia.

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu Bruno Ferry akishirikiana na Yusuph Dabo ina kibarua cha kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kugotea nafasi ya pili kwenye msimamo.

Tabia Maulid Mwita Waziri wa Vijana, utamaduni na michezo ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa jezi mpya Azam FC visiwani Zanzibar.

Taarifa kuhusu uzinduzi wa Azam FC ilitolewa mapema Julai 31 na mpango kazi ilikuwa ni Dar katika boti ya Azam Marine Kilimanjaro VIII, (The Falcon Sea) saa 3:00 saa 9:00 alasiri utazinduliwa Michenzani, Mali, Unguja visiwani Zanzibar.

Tayari Simba ambayo itakuwa na tamasha lake la Simba Day Agosti 3 2024 Uwanja wa Mkapa imekamilisha uzinduzi wa uzi mpya ilikuwa Morogoro katika hifadhi za Mikumi na sasa upo sokoni.

Yanga nao mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24 tayari wamefanya uzinduzi wa uzi wao walipokuwa Afrika Kusini kwenye maandalizi ya kuelekea msimu wa 2024/25 nao upo sokoni pia.

Unauonaje Uzi wao?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live