Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu hapa udhaifu wa Yanga, Ambangile auanika!

Yanga Avic Vs Mamelodi Huu hapa udhaifu wa Yanga, Ambangile auanika!

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha na mchambuzi wa boli, George Ambangile ameutaja udhaifu wa Yanga SC ambao amesema, mwalimu anatakiwa kuufanyia kazi kuelekea mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns.

Ambangile amesema, Yanga wanapokuwa na mpira wana udhaifu wa kuacha nafasi kubwa kutoka kwa mstari hadi mstari wa ukabaji jambo ambalo lina madhara makubwa kama mshindani.

"Hilo labda ndio wanapaswa Yanga kulifanyia kazi maana huwa wanaposhambulia, mabeki wao wa pembeni huwa wanakwenda mbele hivyo kuwaacha nyuma Job, Bacca na Aucho kama atakuwa fiti, ni rahisi sana kushambuliwa na kufungwa kama mtu akipitia katikati yao," alisema Ambangile.

Yanga atawakaribisha Mamelodi Marchi 30, 2024 katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live