Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huu hapa mtihani mgumu kwa Guede

Joseph Guede Yanga Huu hapa mtihani mgumu kwa Guede

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitu pekee kitakacholipa uzito jina la straika wa Yanga, Joseph Guede ni kufunga mabao kama anavyosema staa wa zamani wa timu hiyo, Mohammed Hussein 'Mmachinga'

Yanga ilimsajili Guede kama mchezaji huru baada ya kuachana na Tuzlaspor ya Uturuki, lakini tayari nyota huyo kacheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar akikipiga kwa dakika 33 na Dodoma Jiji ambao alikabiliana nao kwa dakika 90, lakini hajafunga bao.

Mmachinga baada ya kumtazama mchezaji huyo kwenye michezo hiyo hajaona jambo la kumshtua, hivyo kaamua kujipa muda kuona labda akicheza mechi tano huenda akafanya jambo la kuwafanya mashabiki wafurahie huduma yake.

Staa huyo wa zamani mwenye rekodi ya kufunga mabao 26 katika msimu mmoja aliyofunga 1999, amesema: "Guede ili aondoe maswali ya mashabiki wapo wanaoamini wamepigwa, wengine wanaona ni jembe, ni yeye kuanza kufunga mabao.

"Kiufundi wanaocheza nyuma yake na pembeni wajue kumtengenezea mipira ambayo atakuwa anafunga tu na asiwe na mambo mengi uwanjani."

Kitendo cha kumfananisha Guede na straika wa zamani wa timu hiyo, Fiston Mayele ambaye ndani ya misimu miwili alifunga mabao 33, Mmachinga anaamini kinambebesha mzigo mzito.

"Ndio maana naona apewa mechi kama tano, tuone atafanya kitu gani, ila asifananishwe na Mayele ambaye ameifanyia mengi Yanga," amesema.

Yanga leo inacheza na Mashujaa ambayo imepanda Ligi Kuu msimu huu, lakini akipangwa Guede huenda akafunga na kuanza kuwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live