Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hutaki! Liverpool Bingwa EPL

DFSDFG Hutaki! Liverpool Bingwa EPL

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool itashinda ubingwa wa Ligi Kuu England mbele ya Manchester City na Arsenal, imetabiri SunSport.

Miamba hiyo mitatu imetofautiana kwa pointi moja tu kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England huku kila timu ikiwa imebakiza mechi 10 za kucheza kwenye kutambua nani atakuwa bingwa wao.

Bao la dakika za mwisho la Kai Havertz alilofunga kwa kichwa dhidi ya Brentford kwenye ushindi wa mabao 2-1 ulikifanya kikosi cha Arsenal chini ya Kocha Mikel Arteta kushika usukani wa ligi hiyo.

Kisha Jumapili, Liverpool na Man City zilitoka sare ya bao 1-1 uwanjani Anfield na bao la John Stones la kuongoza lilisawazishwa na Alexis Mac Allister kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili.

Matokeo hayo yamefanya Arsenal sasa kuongoza ligi kwa pointi 64, sawa na Liverpool, lakini The Gunners ina wastani mzuri wa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mabingwa watetezi, Man City wao sasa wapo nyuma kwa pointi moja, wakati wakipambana kuhakikisha wanaweka historia ya kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu England kwa msimu wa nne mfululizo.

Hata hivyo, ni Kocha Jurgen Klopp - ambaye huu utakuwa msimu wake wa mwisho Liverpool - waandishi wa SunSport, Rob Maul na Will Pugh wanaamini atanyakua ubingwa wakati msimu utakapofika mwisho Mei 19.

Klopp, ambaye ataachana na Liverpool mwisho wa msimu, atatamani sana kushinda ubingwa wa ligi msimu huu ili iwe mara ya pili kwake, huku ikizingatia mwaka 2020 alishinda kwenye kipindi cha Uviko 19.

Hata hivyo, kwa ratiba ya mechi zilizobaki, Liverpool bado ina shughuli pevu ya kuzikabili timu mahasimu, Manchester United na Everton, huku wakiwa na kipute pia na Tottenham na Aston Villa.

Lakini, itakuwa na mechi za nyumbani dhidi ya Brighton, Sheffield United, Crystal Palace na Wolves.

Arsenal nao watakuwa na ugumu kwenye mechi tatu katika ratiba yao, wakikabiliwa na Man City, Spurs na Man United. Watakuwa na mechi ngumu pia kuwakabili Brighton, Aston Villa na Chelsea.

Kwa upande wao Man City, inayonolewa na Pep Guardiola itakuwa na mechi zijazotaka ujanja mwingi, ambapo watakipiga na Arsenal, Villa na Tottenham. Lakini, kwenye ratiba yao kuna mechi nne za mwisho zinazowapa matumaini wakikabiliana na Nottingham Forest, Wolves, Fulham na West Ham.

Kwa ratiba ilivyo, Man City inaonekana kuwa na nafuu na nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa, lakini SunSport inaamini ni Liverpool ndiyo itakayonyakua taji hilo kwa msimu huu wa 2023-24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live