Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hussein Kazi kupewa 'thank you' na Simba

Hussein Kazi Exchange Hussein Kazi kupewa 'thank you' na Simba

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa kati wa Klabu Simba SC Husein Kazi inatajwa kuwa ni sehemu ya kukamilisha dili la Usajili la Mlinzi wa kati wa klabu ya Coastal Union Lameck Lawi

Imeelezwa kuwa, Simba SC imetoa Kiasi cha pesa pamoja na Hussein kazi ili kukamilisha dili hilo ambalo lilikuwa la wengi kuelekea soko la usajili

Haikuwa rahisi kwa Klabu ya Coastal Union kutupilia mbali ofa za Vilabu vya Ihefu na Azam FC ambao nao walituma ofa ya kumtaka Lameck Lawi

Hussein Kazi amesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu, ambapo alitazamiwa kutoa ushindani kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kwenye timu hiyo hali ambayo ni kama imeshindikanika

Simba wanatazamia kufanya maboresho makubwa ya kikosi chao kuelekea msimu ujao haswa mara baada ya kufanya vibaya msimu huu

Inataarifiwa kuwa moja ya maeneo ambayo Simba SC wanaweza kufanya vyema ni pamoja na usajili wa beki, kiungo na mshambuliaji huku eneo la ufundi wakitazamia kuleta kocha mwenye rekodi kubwa kuja kufanya kazi na Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live