Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hussein Kazi hakuandaliwa kwa dabi - Mchambuzi

Hussein Kazi Asadx Kazi hakuandaliwa kwa dabi - Mchambuzi

Mon, 22 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa michezo Chisano Jr amesema Beki wa Simba SC, Hussein Kazi hakuandaliwa kucheza Dabi.

Chisano amesema hayo baada ya Simba kukubali kichapo kingine cha bao 2-1 kutoka kwa watani zao Yanga kwenye mchezo uliopigwa juzi Aprili 20, katika Dimba la Mkapa huku bao la kwanza likisababishwa na Kazi aliyechukua nafasi ya Inonga, kumchezea rafu Aziz Ki ndani ya boksi la 18.

"Nakumbuka katika mchezo wa FA ambao yanga walipoteza mbele ya Simba kwa mabao 4-1 Kocha alilazimisha kuwachezesha wachezaji ambao wametoka katika majeruhi Haruna Niyonzima na Pappy Tshishimbi,

"Mimi naamini kama kijana Hussein Kazi angeaminiwa kama atakuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa kweye ule mchezo pengine wangebadilika kuanzia katika eneo la ulinzi lakini kuingia kwake kumetumika kama Surprise ya yeye kucheza dabi angeandaliwa asinge kuwa na makosa mengi katika mchezo ule," amesema Chisano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live