Licha ya kutopata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza cha Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’, Beki wa timu hiyo, Hussein Kazi, amesema hana presha na anaimani ipo siku atapata namba na mashabiki wataliimba jina lake.
Kazi amesajiliwa na Simba SC akitokea Geita Gold FC kwa lengo la kuongeza nguvu katika safu ya ulinzi ambayo kwa sasa inaongozwa na Henock Inonga na Che Fondoh Malone.
Kazi amesema anaamini muda wake wa kucheza katika kikosi cha kwanza haujafika na anaahidi nafasi hiyo ikipatikana ataonyesha kiwango kuzuri kitakacho mshawishi Robertinho.
Kazi amesema kwa sasa anaendelea kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa wachezaji aliowakuta na wenye uzoefu huku akiwaambia mashabiki waendelee kuwa na subira.
“Naamini siku yangu itafika na nitapata namba katika kikosi cha kwanza, hayo ni malengo yangu na ninazidi kujiimarisha, kwa muda mfupi niliokaa hapa nimejifunza mambo mengi katika kujijenga,” amesema Kazi.