Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu ya Chama Manungu leo

Chama Clat Kiungo wa Simba, Clatous Chama

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MASHABIKI wa soka wa Simba wana kiu kubwa ya kumuona nyota wao aliyerejea kikosini, Clatous Chama akiliamsha, lakini nyota wa zamani wametaka kiungo huyo fundi apewe muda wa kuonyesha makali yake kama alivyokuwa awali.

Chama aliondoka Msimbazi mwishoni mwa msimu uliopita sambamba na Luis Miquissone wakiuzwa klabu za RS Berkane ya Morocco na Al Ahly ya Misri, lakini Chama amerejea baada ya kukosa namba katika klabu iliyomnunua.

Tayari mashabiki wamekuwa na kiu ya kumuona uwanjani baada ya kumkosa kwa muda mrefu na huenda akaanza kazi kwesho dhidi ya Mtibwa Sugar na nyota wa zamani wa kimataifa nchini kwa nyakati tofauti wamemchambua kiungo huyo.

Beki wa zamani wa Simba Boniface Pawassa alisema, urejeo wa Chama una faida na hasara kutokana na uchezaji wake timu iwapo na mpira au isipokuwanao.

“Faida na hasara za Chama ni pale timu inapokuwa na mpira kitaalamu tunahita without ball (bila mpira) and with ball (ukiwa na mpira) hapo ndipo utakapoona udhaifu wa Chama wakati timu ina mpira utampenda ila ikiwa haina mpira utamkataa,” alisema Pawasa naye Zamoyoni Mogella alisema, mashabiki wa mpira wanatakiwa kuwa na subra na wampe muda Chama kwa muda aliotoka anaweza akawa amebadilika kwa kuwa huko alipoenda hakuweza kupata nafasi mara kwa mara.

“Mashabiki wa mpira sio wa kuwaamini ni miezi sita hivi toka ameondoka, wasitarajie atarudi na ubora ule ule ila wampe subira kuona kiwango chake kama ni kile kile au lah, na kama sio wasimbeze,” alisema Mogella.

Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ alisema Chama na Luis waliondoka na historia fulani, hivyo Simba walitakiwa kuwarejesha wote wawili kutokana na mchango waliokuwa nao kwa pamoja.

“Wangewarudisha wote wawili ingekuwa sawa, kumrudisha Chama ni kama kumtega kwani hakuna mwenye uhakika wa ubora wake au anaocheza nao wanaweza kumpa ubora kama alivyokuwa na Luis,” alisema Mmachinga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live