Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hukumu mashtaka 115 ya Man City kitendawili

City452604801 Hukumu mashtaka 115 ya Man City kitendawili

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imebainika kuwa kati ya mashtaka 115 ya uvunjaji wa kanuni za Ligi Kuu England, imebainika kuwa 80 kati ya hayo yanahusu uvunjaji wa kanuni zinazohusu matumizi ya fedha huku 35 yakiwa ya kiutawala huku hatima ya uamuzi wake ikiwa haijulikani.

Hilo limebainika katika kipindi ambacho Manchester City inakaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL), ikiwa inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa kukusanya pointi 88 ambapo inahitaji ushindi tu katika mechi ya mwisho dhidi ya West Ham ili itwae ubingwa.

Man City ilianza kuchunguzwa juu ya uvunjaji wa kanuni hizo tangu 2019 lakini jarida la Del Spiegel mwaka jana likakoleza moto kwa kufichua kuwa klabu hiyo imehusika na makosa 115 ya kuvunja kanuni za Fedha kwenye EPL.

Hata hivyo, wakati mashauri hayo yakiwa mezani, ripoti mpya imeainisha aina ya makosa ambayo Man City imeyafanya huku yakiwa sio yote yanahusiana na masuala ya fedha.

Kati ya makosa hayo 116, makosa 54 ni ya kushindwa kuwasilisha taarifa sahihi za fedha kuanzia msimu wa 2009/2010 hadi 2017/2018 na makosa 14 ni ya kutowasilisha taarifa sahihi za malipo ya mchezaji na meneja kuanzia msimu wa 2013/2014 hadi 2017/2018.

Makosa matano ni ya kutotii matakwa ya sheria ya matumizi ya usawa ya fedha ya Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa) na makosa saba ni ya kuvunja kanuni ya faida na muendelezo (PSR) na makosa 35 ni ya kutotoa ushirikiano kwa bodi ya ligi England wakati wa uchunguzi kuanzia Disemba 2018 hadi Februari 2023.

Ukirudi nyuma katika uchunguzi wa Der Spiegel, tuhuma zilihusu uingizaji wa fedha kwenye klabu kutoka kwa mmiliki Sheikh Mansour kupitia mikataba ya kijanja, kumlipa fedha meneja Roberto Mancini ili awe kama mshauri wa klabu huko Abu Dhabi lakini pia kuwapa fedha za ziada wachezaji zaidi ya zile zilizokuwa zinaenda kwenye akaunti.

Kinadharia hiyo inaonekana iliruhusu Man City kusajili wachezaji bora na wengi zaidi ya wale ambao ingeweza kuwasajili.

Katika kipindi ambacho kimehusishwa na City kufanya makosa hayo, timu hiyo ilishinda Ligi Kuu ya England 2012 na 2014, kumaliza katika nafasi ya pili mara mbili, kuchukua kombe la FA mara moja na kufungwa katika fainali ya mashindano hayo mwaka 2013 na pia kufika fainali ya kombe la EFL mwaka 2014 na 2016.

Bila kupata fedha za ziada mjadala unaenda mbali na kudai kwamba Man City isingeweza kushinda kile ilichopata na isingeweza kupiga hatua kufikia pale ilipokuwa wakati Pep Guardiola anawasili 2016 na kuigeuza kuwa timu yenye mafanikio zaidi duniani, akiwawezesha kushinda mataji matatu kwa mpigo 2023.

Kuna namba ya maofisa wa klabu wakiwemo, mkurugenzi Simon Pearce, mtendaji mkuu, Ferran Soriano, mwenyekiti Khaldoon al-Mubarak na mmiliki Sheikh Mansour ambao ushiriki wao ulikuwa na mchango mkubwa.

Ni sawa pia kwa mtendaji mkuu mpya wa Manchester United, Omar Berrada aliyefanya kazi katika kampuni ya City Group katika masuala mbalimbali kuanzia 2011 na kukubaliana dili nyingi.

Hukumu kizungumkuti

Suala la lini uamuzi juu ya mashtaka yanayoikabili Man City yatatolewa uamuzi linaonekana kuwa sintofahamu ambayo inafanya wengi kutilia shaka mamlaka ambazo zinachunguza na zinapaswa kumaliza kesi hizo.

Hadi sasa hakuna anayefahamu lini majibu juu ya mashtaka ya Man City yatatolewa majibu na kama wataadhibiwa iwapo watakutwa na hatia.

Kumekuwa na taarifa kuwa tarehe ya usikilizwaji wa mashtaka hayo itakuwa ni wakati wa msimu wa kipupwe baadaye mwaka huu huku tarehe ya uamuzi ikitajwa kuwa wakati wa majira ya kiangazi 2025.

Man City ina kumbukumbu ya kushinda kesi kama hizo ambapo iliwahi kuishia kutozwa faini ya Euro 10 milioni na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa michezo (Cas) na kupindua adhabu ya kufungiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili ambayo ilipewa na Umoja wa Vyama vya Mpira wa Miguu Ulaya (Uefa).

Klabu hiyo ilikubaliana na uamuzi wa Cas kwa vile ilidai haina imani na Uefa ingawa tuhuma nyingi zilitupiliwa mbali na Cas kwa vile mahakama hiyo ilisema kuwa ziliwasilishwa nje ya muda.

Meneja wa Manchester City, Pep Guardiola ni miongoni mwa wanaotamani kuona mashauri hayo yanasikilizwa na uamuzi unatolewa mapema akidai itasaidia kuisafisha klabu yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live