Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Simba moto ni mzito, mashabiki waombwa utulivu

Simba Ahmed Mashabiki Ahm

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amewaomba mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuungana na kuwa wamoja.

"Jana tumepokea taarifa mbili kubwa na muhimu ndani ya klabu yetu. Kila mmoja anajua amepokeaje taarifa hizo iwe kwa furaha au huzuni, lakini taarifa mbili za jana ni kwa maslahi na ustawi wa klabu yetu pendwa ya Simba.

"Nichukue nafasi hii kuwaomba Wana Simba, Tuungane na kuwa kitu moja, tuache malumbano na turudi katika misingi yetu ya Nguvu Moja. Mbele yetu tuna matukio muhimu ambayo yanahitaji umoja, utulivu na ushirikiano ili kuyafanikisha.

"Ndani ya miezi miwili hii 6-8, Tuna Usajili, Pre Season, Simba Day, Ngao ya Jamii, Kagame Cup na Ligi Kuu matukio yote haya tunapaswa kuyaendea tukiwa wamoja ili tuweze kufanikiwa.

"Ni wakati sasa wa kuondoa tofauti zote sanjari na kuwapa Ushirikiano viongozi wetu waliopo madarakani

"Kwa wale wana Simba wanaopata nafasi ya kutoa maoni kwenye vyombo vya habari basi tujikite kwenye kuhamasisha Umoja, Mshikamano na Utulivu. Sisi sote ni Simba na lengo letu ni kuona Simba inafanya vizuri. Mungu Ibariki Simba Sports Club."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live