Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Mtibwa kicheko tu, waivimbia KMC

IMG 7213 Mtibwa Vs .jpeg Huko Mtibwa kicheko tu, waivimbia KMC

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila akichekelea kuanza kibarua chake kwa kishindo, straika wa timu hiyo Seif Karie naye amekoshwa na kiwango chake akisema sasa ndio wameianza Ligi Kuu.

Katwila akiiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu, waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Geita Gold na kujinasua mkiani hadi nafasi ya 13 kwa pointi tano baada ya mechi saba.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo sita chini ya aliyekuwa kocha mkuu, Habibu Kondo aliyetemwa kufuatia matokeo yasiyoridhisha.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro, mabao ya Karie (mawili) na Ladack Chasambi huku la Geita Gold akijifunga Kipa wao, Mohamed Makaka.

Akizungumza Karie amesema huo ulikuwa mchezo wake wa pili msimu huu na mabao yake ya kwanza akichekelea kiwango alichoonesha na kuipa ushindi timu yake.

Amesema baada ya ushindi huo kwa sasa morali na matumaini yamekuwa makubwa kikosini akitamba kuwa wanaenda kujipanga tena na mechi ijayo dhidi ya KMC, Oktoba 31 huko Dar es Salaam.

“Japokuwa sijacheza dakika zote 90 kila mechi, lakini nashukuru kwa kiwango leo (juzi) lakini kuipa ushindi timu yangu ni furaha kubwa zaidi, kwa sasa ari, morali na nguvu imerejea upya,”

“Tunaenda kujipanga upya kuhakikisha tunaendeleza ushindi katika mchezo ujao dhidi ya KMC, haijalishi tupo ugenini kimsingi ni pointi tatu ili kufikia malengo,” amesema nyota huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: