Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Ligue 1, ukizingua, umepotea

Mbappe X Enrique Huko Ligue 1, ukizingua, umepotea

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

NI wikiendi nyingine kwenye mwendelezo wa Ligi Kuu Ufaransa. Huko kutakuwa na mechi nane zitakazopigwa kwenye viwanja vinane tofauti, lakini jambo gumu ni kwamba timu yoyote ikizingua inaweza ikajikuta kwenye nafasi tatu chini na zile zitakazoshinda zina nafasi ya kupanda zaidi ya nafasi tatu.

Ukianzia pale juu, kuanzia kwa Monaco iliyo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42, Lille nafasi ya nne yenye alama 41, Nice nafasi ya tano kwa alama zao 40 na Lens iliyo nafasi ya sita na alama 39, zote hizi zinaweza kupanda na kushuka kwa kupoteza ama kushinda mechi za wikendi hii.

Kuanzia timu ya tatu hadi sita utofauti wa alama ni mbili tu. Hivyo timu yoyote itakayopoteza inaweza kujikuta matatani. Ukiondoa ushindani uliopo kwenye zile nafasi za juu, pia hata timu zilizo kwenye nafasi za chini mambo ni moto.

Kuanzia kwa Montpellier, iliyo nafasi ya 16 kwa pointi zao 23, hadi kwa Toulouse inayoshika nafasi ya 10, zote zinaweza kubadilishana nafasi wiki hii ikiwa moja wapo itapoteza na nyingine kushinda.

Chanzo: Mwanaspoti