Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Kaitaba kuna vita nzito

Kaitaba Pic Data Huko Kaitaba kuna vita nzito

Mon, 26 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KUNA vita moja kubwa ya Ligi Kuu Bara leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Karume, mjini Musoma Mara ambapo wenyeji Biashara United wataikaribisha Kagera Sugar, huku wakitamba hata iweje wageni wao hawachomoki.

Timu hizo zinakutana kwenye uwanja huo huku mchezo unaotarajiwa kuwa mgumu na wenye mvuto huku sababu kubwa ikiwa ni jinsi Kocha Francis Baraza alivyoondoka ghafla Biashara na kujiunga na Kagera.

Baraza aliiacha Biashara ikiwa nafasi ya nne, lakini tangu aondoke timu hiyo imecheza mechi nne, ikipoteza mbili na kutoka sare mbili na sasa ina pointi 41.

Kuondoka kwa Baraza ndani ya Biashara kuliwaumiza sana si tu viongozi wa timu hiyo bali hata wachezaji kwani hawakulitegema.

Sasa timu hizo zinakutana kesho huku kocha msaidizi wa Biashara, Marwa Chamberi akikiri itakuwa mechi ngumu na ya kibabe ila hawatakubali wapoteze pointi.

“Itakuwa mechi kama dabi vile maana tunakutana na bosi wetu wa zamani, anaijua vizuri hii timu na anafahamu uwezo wa kila mchezaji, ila niseme tuko nyumbani na hatuwezi kukubali kufungwa,” alisema Chamberi.

Kocha Baraza alisema anachosubiri ni dakika 90 ndio zitaamua hivyo hana maneno mengi.

“Narudi nyumbani, sehemu niliyokaa muda mrefu, hivyo haitakuwa mechi rahisi. Ngoja tusubiri dakika 90 ndizo zitaamua huu mchezo ,” alisema Baraza.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz