Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko First League ni kivumbi na jasho

First Leagueeeeee Huko First League ni kivumbi na jasho

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati First League ikianza kurindima wikiendi iliyopita, timu za Malimao, Kiluvya, TRA na Tanesco zimeanza vyema michuano hiyo baada ya kufanya kweli dhidi ya wapinzani.

Ligi hiyo ambayo inashirikisha timu 16 ambazo zimepangwa makundi mawili tofauti, ilianza kutimua vumbi Jumamosi na jana Jumapili kwa mechi saba, huku mbili zikishindwa kufanyika.

Katika mechi za kwanza zilizopigwa viwanja tofauti nchini, Mapunduzi ya jijini Mwanza ikiwa ugenini iliichachafya Kurugenzi ya Simiyu 2-0, huku TRA nao wakishinda idadi hiyo dhidi ya Alliance FC, mabao ya wakusanya kodi hao yakiwekwa wavuni na Husein Kaoneka dakika ya 20 na Oscar Tarimo dakika ya 29.

Tanesco nao wakiwa ugenini walifanya kweli kwa kuwakanda mabao 2-0 Kasulu United, mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, huku mechi ya African Lyon na Nyumbu ikishindwa kufanyika.

Katika mechi za jana Jumapili, Malimao ikiwa nyumbani jijini Dar es Salaam, iliifanyia kitu mbaya Tunduru Korosho kwa kuizabua 3-0, shukrani kwa mabao ya Salum Kifigo, Ahmad Hassan na Mohamed Matili.

Kiluvya nao wakicheza katika ubora wao walifanya kweli kwa ushindi wa 3-0 mbele ya Dar City, ilhali mechi baina ya Nyumbu na African Lyon ikipigwa kalenda.

Nahodha wa Rhino Rangers, Ntilakigwa Hussein amesema kuanza kwa ushindi ugenini unaongeza ari na morali kubwa kikosini na kwamba malengo yao ni kuirejesha timu hiyo championship.

“Tunawashukuru mashabiki kwa sapoti yao na matokeo haya ni chachu kwetu katika kuendelea kuipigania timu kuhakikisha inarudi championship na hatimaye Ligi Kuu,” amesema Hussein.

Naye Meneja wa Malimao, Idd Mwambusi amesema pamoja na ugeni wao kwenye michuano hiyo, lakini matokeo hayo ni dalili njema kwao katika kufikia malengo ya kupandisha timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti