Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Championship moto umewaka

Championship Pic Huko Championship moto umewaka

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Championship msimu wa 2023/24 ikitarajia kuanza Septemba 9, vita itakuwa nzito katika kusaka timu mbili za kupanda Ligi Kuu moja kwa moja, huku nyingine ikijitetea kwenye play off.

Awali ligi hiyo inayotoa timu za kupanda Ligi Kuu Bara, ilipangwa kuanza Jumamosi, lakini ikaahirishwa kwa wiki moja ili kuzipa nafsi klabu kujiandaa kwani ratiba ilichelewa kuachiwa na Bodi ya Ligi kabla ya kalenda ya michuano hiyo kuanza.

Msimu uliopita ulionekana kuwa na neema kwa timu za championship baada ya kupandisha tatu ikiwa ni rekodi ya pili ikiwamo msimu wa 2020/21 tangu kuanzishwa kwa kanuni ya play off.

Katika msimu huo ambao championship ikiitwa daraja la kwanza ilikuwa katika makundi mawili na Gwambina na Dodoma Jiji zilipanda moja kwa moja, huku Geita Gold na Ihefu zikicheza play off.

Geita Gold iliyokuwa nafasi ya pili kwenye kundi A ilicheza dhidi ya Mbeya City na ilipoteza kwa jumla ya mabao 2-1 huku Ihefu ikipanda kwa faida ya mabao mawili ya ugenini ikiishusha Mbao iliyoshinda nyumbani 4-2, japokuwa ilipoteza awali 2-0.

Rekodi hiyo ilikuwa ya kwanza kupata timu ya championship kupanda kupitia mchujo ‘play off’ kwa kuwafunga wapinzani Ligi Kuu, jambo ambalo limejirudia tena msimu uliopita.

Katika msimu wa 2022/23, ilishuhudia timu za JKT Tanzania na Kitayosce zikipanda moja kwa moja baada ya kuongoza nafasi mbili za juu, lakini Mashujaa wakifuata nyayo za Ihefu kwa kuwashusha Mbeya City kwa jumla ya mabao 5-1.

Kwa sasa kinachosubiriwa na wadau na mashabiki ni kuona nani watachanga vyema karata ya kucheza Ligi Kuu msimu wa 2024/25 kwa wababe 16 kupepetana.

Msimu ujao mbali na ubora wa vikosi na maandalizi ya jumla, kazi itakuwa kwa makocha kutokana na baadhi ya timu kuvunja benki kupata saini zao kwa lengo la kupanda Ligi Kuu.

Mbali na vita ya makocha, kutakuwa na ishu ya ukanda kila upande ukitamani kuwa na timu ya Ligi Kuu, lakini usajiliwa majina makubwa nao utakuwa na sehemu yake.

Jumanne Challe

Ken Gold ambayo inatarajia kushiriki kwa msimu wa nne ligi hiyo, awali iliamua kumpa kazi nyota wa zamani wa Simba na Taifa Stars mwenye rekodi yake, Amri Said ‘Stam’ kabla ya kocha huyo kuchomoa na sasa ametua Lipuli iliyonunua Ruvu Shooting.

Challe anaiongoza timu hiyo tajiri yenye uchumi wake na makazi huko wilayani Chunya zilipo dhahabu akichukua nafasi ya Stam aliyekaa nao muida mfupi kuchukua mikoba ya Ngawina Ngawina aliyechomoka hapo mwishoni mwa msimu uliopita.

Kocha huyo mwenye misimamo yake anakumbukwa kazi zake akiinoa Simba, Lipuli, Mbao, Mbeya City na KVZ ya Zanzibar kwa mafanikio na sasa anasubiriwa kuona maajabu yake kikosini humo, hivyo kuondoka kwake kwelnda Lipuli ni kama amemwachia msala Challe ambaye hata hivyo ana uzoefu wa ligi hiyo.

Mayanga

Kocha Salum Mayanga ndiye ameshikilia matumaini ya wadau na mashabiki wa soka jijini Mbeya kila mmoja akisubiri kazi yake ya kuirejesha Mbeya City Ligi Kuu.

City ilishuka daraja msimu uliopita ikiwa chini ya Kocha Abdalah Mubiru, raia wa Uganda na sasa kibarua kipo kwa Mayanga ambaye rekodi zake hapa bongo kila mmoja anazijua.

Mayanga nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Taifa Stars amewahi kuzifundisha timu kadhaa kwa mafanikio ikiwamo Mtibwa Sugar, Tanzania Prisons na Kagera Sugar.

Makata

Pamba Jiji FC ambayo imesota kwa miaka kibao bila kupanda daraja tangu iliposhuka mwaka 2000, imemwamini Kocha Mbwana Makata kuwaondolea aibu hiyo kwa jiji hilo kubwa nchini.

Makata ambaye amezifundisha na kuzipandisha timu kadhaa, kwa sasa macho ya wana Mwanza yapo kwake kuhakikisha anawapelekea uhondo wa Ligi Kuu walioukosa kwa misimu mitatu sasa.

Mwanza haina timu ya Ligi Kuu tangu timu za Gwambina, Toto Africans, Mbao na Alliance FC ziliposhuka daraja kwa misimu tofauti, huku Pamba ikisota championship kwa zaidi ya miaka 10.

Wengine ni Ngawina Ngawina anayeinoa TMA iliyopanda daraja kwa mara ya kwanza, Maka Mwalwisi (Mbeya Kwanza) na Leonard Budeba (Mbuni FC) na Amani Josiah anayeiongoza Biashara United.

Kanda ya Ziwa

Kanda hiyo yenye mambo mengi katika medani za soka, msimu ujao itawakilishwa na timu nne, Pamba Jiji, Copco Stand United na Biashara United ambazo zina historia yake nchini.

Biashara United iliyowahi kucheza Ligi Kuu kabla ya kushuka daraja misimu mitatu nyuma, kwa sasa inajitafuta tena kuhakikisha inarejesha uhondo kwa mashabiki wake mjini Musona mkoani Mara.

Katika kuhakikisha inafanya kweli, imemrejesha kikosini kocha Josiah aliyepanda nayo msimu wa 2019/20 akisaidiwa na Edna Lema aliyewahi kuifundisha Yanga Princess.

Kwa upande Pamba Jiji, msimu ujao itakuwa katika mwonekano wa tofauti baada ya kukabidhiwa katika mikono ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza tofauti na ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma.

Timu hiyo kongwe iliyowahi kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano mwaka 1999 na kushuka daraja mwaka 2000, ipo mikononi mwa kocha Makata na msaidizi wake, Renatus Shija.

Matarajio ya wengi ni kuona ‘TP Lindanda’ yenye idadi kubwa ya mashabiki nchini na ushawishi mkubwa kwa wadau ikirejea Ligi Kuu na kurudisha heshima yake na Mkoa kwa jumla.

Stand United ‘Chama la Wana’ yenye mzuka mwingi mjini Shinyanga, baada ya kupotea kwa muda mrefu wamerejea kupambania nafasi yao ya Ligi Kuu waliyoikosa kwa misimu kadhaa.

Nyanda za Juu Kusini

Moja ya kanda ambayo haipoi wala kuboa ni pamoja na nyanda za juu kusini ambayo huwa haiishiwi timu kwenye Ligi Kuu wala Championship na msimu ujao itakuwa nazo nne, hii n ui baada ya ununuzi wa Ruvu Shooting na kubadilishwa jina na kuwa Lipuli ambayo amepewa Jaap Stam aliyewahi kuinoa kipindi ikicheza Ligi Kuu Bara na kutisha.

Mkoa wa Mbeya ndio unawakilisha kanda hiyo ikiwa na timu hizo, Mbeya City, Ken Gold na Mbeya Kwanza licha ya kwamba baadhi hazitatumia uwanja wa Sokoine zikitafuta sehemu nyingine.

Mbeya Kwanza kama ilivyo kawaida yake, msimu ujao itakuwa mkoani Mtwara ikitumia Uwanja wa Nangwanda Sijaona, huku wenzake wakibaki jijini Mbeya kwa mechi zao za nyumbani.

Kaskazini na Kati

Huko Kanda ya Kaskazini kipute kitakuwa kwa miamba watatu ambao ni Maafande, Polisi Tanzania, TMA na Mbuni FC zote zikiwakilisha Kilimanjaro na Arusha katika Championship msimu ujao.

TMA FC ambao wanashiriki ligi hiyo kwa mara ya kwanza ikiwa chini ya Kocha Ngawina, huku Mbuni wakishiriki kwa msimu wa tatu na kila mmoja anapigania nafasi ya kucheza Ligi Kuu.

Polisi Tanzania wao walishuka daraja msimu uliopita na wanajitafuta tena kimya kimya kuhakikisha wanarejea upya licha ya ushindani uliopo kwenye Championship. Mbuni wao licha ya kucheza ligi hiyo kwa misimu mitatu bila mafanikio, wanafikiria huenda mwaka huu ukawa na neema kwao kupanda Ligi Kuu na kuweka historia kwao.

Huko kanda ya kati itakuwa na timu moja, Fountain Gate ambao licha ya upinzani wao kwenye michuano hiyo lakini hawajaonja ladha ya Ligi Kuu wakiamini msimu huu lolote linaweza kuwatokea.

Mashariki

Kanda ya Mashariki itakuwa na wababe watano, Dar City, Cosmopolitan, Transit Camp, Green Warriors na Pan Africa ambao kila mmoja anasaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao na kuweka heshima.

Dar City haijawahi kucheza Ligi Kuu sawa na Trans na Green Wariors, huku Cosmopolitan na Pan African wakiwa wameikosa ligi hiyo kwa miaka zaidi ya kumi hivyo kufanya msimu ujao kuwa wenye upinzani mkali.

Wasikie makocha

Kocha mkuu wa Mbeya City, Salum Mayanga anasema timu yake si ya kushiriki championship bali kupanda Ligi Kuu akitamba usajili uliofanywa unatosha kufikia malengo.

“Hii ni timu ya kupanda Ligi Kuu, tumesajili wachezaji 25 ambao kila mmoja ana uwezo wake, kimsingi ni ushirikiano na kujituma ndani na nje ya uwanja kufikia malengo,” anasema Mayanga.

Kocha mkuu wa Ken Gold, Amri Said ‘Stam’ anasema pamoja na upinzani wanaotarajia kwa timu shiriki lakini misimu minne ya timu hiyo kwenye championship imetosha na sasa wanaitaka Ligi Kuu.

“Tumekuwa na muda wa kutosha kujiandaa, vijana wameonyesha uhai na matarajio ni kupanda Ligi Kuu, championship imetosha sasa,” anatamba Stam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live