Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Bara kuna vita ya ndugu

Ligi Kuu Pic Huko Bara kuna vita ya ndugu

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu imezidi kushika kasi huku Yanga ikitesa kileleni kwenye msimamo kwa alama zake 59 akiwa anausaka ubingwa wake wa pili mfululizo baada ya kubeba msimu uliopita.

Yanga ina vita dhidi ya Simba ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na alama 53 na mchezo ujao itakutana na Azam yenye kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo uliopita uliopigwa Uwanja wa Mkapa bao lililofungwa na Prince Dube.

Simba na Yanga zinatarajia kukutana Aprili 16, mchezo ambao Simba itakua nyumbani na endapo atafanikiwa kupata ushindi atapunguza alama dhidi ya mpinzani wake ambaye hadi sasa amepoteza mchezo mmoja dhidi ya Ihefu ilipofungwa 2-1.

Wakati watani hao wakiwa na vita yao, Kagera Sugar inayoshika nafasi ya nane kwa alama 26 inapambana na Mtibwa Sugar iliyopo nafasi ya tisa huku zote zikiwa na alama sawa.

Mchezo uliopita zilikutana Novemba 28, Kagera ikiwa nyumbani na kupata ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Meshack Abraham na sasa zitakutana mzunguko wa 29 katika Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Vita nyingine kwenye ligi ipo kwa timu zinazomilikiwa na halmashauri, Mbeya City nafasi ya 10 kwa alama 24 sawa na Dodoma nafasi ya 11 huku KMC nafasi ya 12 pointi 23.

Mbeya City itakutana na KMC katika mchezo wa kufunga msimu utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga huku Dodoma Jiji na KMC zitavaana Aprili 22 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Vita kwa timu za majeshi, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ambazo zipo kwenye mstari wa kushuka daraja.

Polisi Tanzania itakutana na Prisons Uwanja wa Ushirika, Moshi katika mchezo ujao wakati Prisons na Ruvu Shooting zitakutana Aprili 16 Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Alama tatu kwa Polisi Tanzania itaishusha Ruvu Shooting na Ruvu ikishinda itaishusha Coastal Union na Wagosi hao wakivuna alama tatu itaishusha Prisons lakini Wajelajela hao wakishinda wataishusha KMC, Dodoma Jiji na Mbeya City japo inategemeana na matokeo yao.

Kocha wa Ruvu Shooting, Mbwana Makata alisema Ligi Kuu bado haina mwenywe lolote linaweza kutokea kama watapata matokeo mazuri kwenye michezo yao ijayo na itabadilisha msimamo.

Kocha wa Polisi Tanzania, John Tamba alisema wao walishaliona hilo mapema ndio maana kila mchezo sasa wanapambana ili kupata alama tatu japo suluhu waliyoipata dhidi ya Kagera Sugar ilivuruga hesabu zao

Chanzo: Mwanaspoti