Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hugo Lloris kuikacha Tottenham Hotspur

Skysports Hugo Lloris Tottenham 4942585 Hugo Lloris

Sun, 7 May 2023 Chanzo: Dar24

Mlinda Lango na Nahodha wa Tottenham, Hugo Lloris amebainisha wazi kuwa huu ni msimu wake wa mwisho kuwepo ndani ya timu hiyo, kufuatia kufanya maamuzi ya kusaka maisha mahala pengine, kuanzia msimu ujao 2023/24.

Kipa huyo kutoka nchini Ufaransa alisajiliwa Klabuni hapo mwaka 2012, akitokea Olympic Lyon, na tayari ameshaitumikia Spurs katika Michezo 361.

Lloris ameongeza kuwa hajisikii tena kuichezea klabu hiyo ya jijini London licha ya kusaliwa na mkataba wa mwaka mmoja.

Kipa huyo kwa sasa yuko nje kutokana na majeraha ambayo aliyapata wakati wa timu ikichapwa kichapo cha kudhalilisha dhidi ya Newcastle United cha mabao 6-1.

Kwa mujibu wa Evening Standard ni kuwa Tottenham italazimika kutafuta Mlinda Lango mpya kwa msimu ujao baada ya Lloris mwenye umri wa miaka 38, kuweka wazi juu ya kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Chanzo: Dar24