Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huenda ndio Machweo ya Feisal Salum

Fei Toto Asd.jpeg Feisal Salum

Mon, 6 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shuleni, tulijifunza kwamba Dunia inazunguka Jua, kwenye mhimili wake na moja ya matokeo yake ni kupatikana kwa mchana na usiku, pamoja na misimu harakati za kuzunguka Kwa Dunia ziligunduliwa mnamo 1543 na mtaalam wa nyota toka Poland Nicolás Copernicus, Katika kitabu chake anaelezea harakati za kila wakati ambazo dunia hufanya wakati inapozunguka kwenye mhimili wake kutoka magharibi hadi mashariki Kwa Masaa 24.

Nikutoe huko nikulete mpaka mitaa ya Jagwani alafu nikurudishe nyuma mpaka Mwaka 2018 ambapo Dunia ilipojizungusha Kwenye mhimili wake Yanga ilifanikiwa kumsajili Bwana Mdogo Feisal Salum Abdalah "FEI TOTO" ambaye alitoka Katika Klabu ya JKU ya Huko kwao Visiwani Zanzibar

Usajili wake hapo awali ulionekana Kuwa ni wakawaida,Lakini Pale Dunia ilipojizungusha Kwenye Mhimili Wake Kila mtu alianza Kuliimba Jina Lake, na wengi Kumwaga Sifa tele Kwa mchezaji huyo ambaye aligeuka kuwa kipenzi cha Klabu hiyo.

Kwa Kiwango ambacho alikuwa akikionesha Kwa wakati ule,na Kuisaidia Klabu yake kutwaa Baadhi ya Vikombe Ikiwemo Kutoa Ukame Wa kushinda kikombe Cha Ligi Kuu [ NBC ] na Vikombe Vingine kama ASFC na Mapinduzi Cup

Lakini Kimbembe Kilianza mwishoni mwa Mwaka 2022 Baada ya Dunia Kujizungusha Kwenye Mhimili Wake Mchezaji Huyo aliyekuwa kipenzi Cha Mashabiki wengi Wa Klabu hiyo Ghalfa Alituma Barua ya kuvunja Mkataba na Kutaka Kuondoka Katika Klabu hiyo

Taarifa iyo Ilimshtua Kila Mmoja,hakuna Aliye Amini Kama mchezaji Huyo Angeweza Kufanya Ivo ghalfa Katikati ya Msimu Kwa Jinsi Alivoipenda Klabu Yao Tena Akiwa na Mkataba na Klabu Hiyo

Hali hiyo ilileta Sintofahamu Kubwa ndani ya klabu na Kwa Mashabiki Wa Timu hiyo, Baadhi yao Walijaribu Kumtafuta na Kumshawishi Lakini Hakuna Kilichobadilisha Msimamo Wa Mchezaji Huyo.

Dunia Ilipojizungusha Kwenye Muhimili Wake na Kuingia Mwaka 2023 Basi Asilimia Kubwa ya wale wote Waliokuwa wakimpenda na kumsifu ikiwemo Mashabiki Wamepoteza Kabisa Mapenzi Nae na Kumtaka Asirudi na Aondoke Kabisa Katika Klabu Yao!

Mpaka Leo Haijulikani Nini Hatima Yake! Nakukumbusha tu Kuwa hayo Yote ni matokeo ya Dunia Kujizungusha Katika Mhimili wake,Hakuna anaejua kesho yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live