Klabu ya Horoya AC imefeli kwenye moja ya kigezo kinachotakiwa ili ijumuishwe kwenye timu (8) za kwanza zitakazoanzisha ligi ya AFRICAN SUPER LEAGUE.
Baada ya ukaguzi uliofanywa na maafisa wa CAF majibu yametoka kwamba, viwanja vyote vya Guinea havina sifa za kohost mechi za mashindano hayo.
Horoya wako hatarini kutolewa kwenye timu (8) zilizochaguliwa awali kuanzisha ligi hiyo.
Klabu zilizochaguliwa ni ;
1. Mamelodi Sundowns 2. Petro de Luanda 3. Tp Mazembe 4. Simba sports club 5. Horoya AC 6. Wydad Casablanca 7. Esperance de 8. Al Ahly
Iwapo Horoya atatolewa klabu nyingine itaongezwa kwenye orodha.