Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Horoya washikilia hatma ya Simba Robo Fainali CAF

Simba Msh.jpeg Simba SC

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanikiwa kuichapa Vipers ya Uganda katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar Machi 7 na kufikisha alama 6 , na kusogea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa kundi C.

Simba sasa inapiga mahesabu makali namna ya kupenya hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo mkikubwa kwa ngazi vya vilabu barani Afrika.

Machi 18 Simba wataikaribisha Horoya kwa Mkapa na hapo ndipo watakapotakiwa kuhakikisha wanachukua alama zote tatu toka kwa Horoya ili kujihakikishia nafasi ya kusonga hatua ya Tobo Fainali kwani ushindi dhidi ya Horoya utawafanya kufikisha alama 9 ambazo sio Horoya wa Vipers watakaokuwana uwezo wa kuzifikia.

Horoya leo Machi 7 wamepokea kichapo cha magoli 3-1 kutoka kwa vinara wa kundi C, klabu ya Raja Casablanca.

Mpaka sasa msimamo wa kundi C upo hivi;

1.Raja Casablanca - 12

2.Simba SC. -6

3. Horoya. -4

4. Vipers FC. -1

Kila timu imeshacheza michezo minne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live