Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homa ya Dabi yaanza mapema

Mashabiki Wa Simba V Yanga Homa ya Dabi yaanza mapema

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wiki moja kabla ya kupigwa pambano la watani wa jadi wa soka nchini, Simba na Yanga, zikikutana kwenye mechi ya 109 tangu Ligi ya Bara iasisiwe mwaka 1965, tayari homa ya pambano hilo imeanza mapema kwa mashabiki wakitambiana mitaani na mitandaoni.

Licha ya mashabiki wa klabu hizo kuliamsha mapema, makocha wa timu hizo Juma Mgunda na Nasreddine Nabi kwa muda tofauti walisema mechi hiyo kwa sasa wanaiweka kiporo ili kuangalia michezo yao ya kimataifa kuona wanatoboa vipi kwenda makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba na Yanga zitavaana Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku zikitoka kwenye majukumu ya mechi za kimataifa zinazozochezwa leo jijini Dar es Salaam na Khartoum Sudan.

Yanga ipo Sudan kurudiana na Al Hilal baada ya sare ya 1-1 nyumbani wakati watani wao watakuwa Kwa Mkapa kumalizana na Primeiro de Agosto ya Angola iliyochapika mabao 3-1 ikiwa kwao katika mechi za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Uwepo wa mechi hizo za kimataifa ndizo zilizochochea mashabiki na wapenzi wa timu hizo kuanza mapema kutambiana kwa kuamini matokeo ya michezo hiyo ya CAF itatoa picha ya timu ipi inaweza kuumia Jumapili ijayo kwenye Kariakoo Derby.

'Sio unachekelea hapa inabidi ufike makundi urudi umbutue Uto, hata usipochukua Kombe ilimradi umemfunga huna raha kiasi cha kuwacheka mzee' anaandika shabiki anayejiita ting????@tingtingVI., huku mwingine aitwae mZoPaNgA@budhabest akiandika kwenye akaunti yake ya twitter; "Wanetu mmewafanya makolo kuongea ovyo kama mashangingi ya Magomeni hembu fanyeni Jambo huko jamani kabla hatuja wavujisha Damu tena trh23'

Hata hivyo, kocha Mgunda, akizungumza mazoezini katika maandalizi ya mechi ya leo dhidi ya Agosto alisema wanamalizana na Waangola kisha ndipo aanze habari za Ligi Kuu, huku Nabi alisisitiza; "Tuna kazi kubwa mbele yetu, hili ndilo tunaloliangalia kwa sasa hizo habari nyingine tukisharudi kutoka Sudan. Tunataka kwenda makundi, kwani itaongeza morali kwa mechi nyingine zijazo."

Chanzo: Mwanaspoti