Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hollwood, Forest zaanza na moto Songwe

Holywood Hollwood, Forest zaanza na moto Songwe

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati Ligi ya Mkoa wa Songwe ikianza kurindima, timu za Hollwood, Inspire na Forest zimeanza vyema baada ya kuzifanyia kitu mbaya dhidi ya wapinzani walioakata utepe wa ligi hiyo.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 14, ilianza kutimua jana kwa mechi tatu ambapo kila upande ukisaka matokeo mazuri kwa lengo la kufukuzia ubingwa wa Mkoa huo na kukta tiketi ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) ili kupanda First League.

Katika mechi ya kwanza ilishuhudiwa Hollwood ambaye ni bingwa mtetezi akitakata mabao 2-0 dhidi ya Sasanda FC, huku mabao ya Jacob Mwalembe na Wiliam Masawe yakizima Sasanda FC.

Kwa upande wa Inspire ikicheza kwa ubora wao katika Uwanja wa Vwawa mkoani humo, iliifumua Maji FC kwa mabao 3-2, shukrani kwa kazi nzuri ya Amani Mkumbwa aliyetupia matatu 'hat-triki' dakika ya 22, 44 na 65, huku Maji ikipata mabao kupitia kwa Daud Msanjili dakika ya 55 na Ezekia Mwazembe dakika ya 57.

Forest nao haikuwa nyuma baada ya kuishindilia Malonji Stars kwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa CCM Vwawa mkoani humo, huku bao la Robert Mboma likitosha kuipa alama tatu timu hiyo.

Kocha Mmkuu wa Inspire, Terry Daniel amesema licha ya ushindi walioanza nao kuwapa morali wachezaji, lakini benchi la ufundi limebaini kuwapo makosa katika eneo la beki kwa kuruhusu mabao mengi.

"Kulitokea makosa yaleyale eneo la beki kupoteza umakini lakini tunaamini tutarekebisha ili mechi inayofuata dhidi ya Hollwood tuweze kushinda mabao mengi bila kuruhusu wavu wetu, ushindi huu umetupa mwanzo mzuri " amesema Daniel.

Chanzo: Mwanaspoti