Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hojlund kuzua utata United

Rasmus Hojlund Atalanta March 2023 1 Rasmus Hojlund

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imeripotiwa kuweka kikomo cha kumsajili Rasmus Hojlund kwa zaidi ya pauni milioni 60 licha ya bei ya Atalanta kutaka pauni milioni 86 huku Mashetani Wekundu wakiwa tayari kutoa dau la kwanza la kumnunua mshambuliaji huyo anaekipiga ligi ya Serie A nchini Italia.

Mshambulizi huyo wa Denmark, 20, anasalia kuwa mchezaji nambari moja anayelengwa na United baada ya kujiondoa kwenye mbio za kumnunua Harry Kane ingawa mmiliki wa Spurs Joe Lewis amemwambia mwenyekiti Daniel Levy kumuuza nahodha huyo wa England msimu huu wa joto ikiwa hatasaini mkataba mpya katika klabu hiyo.

United wamekuwa kwenye mazungumzo na Atalanta kwa wiki kadhaa baada ya kukamilisha mazungumzo ya awali na Hojlund ambaye mpaka sasa bado haijafahamika hatma ya mshambuliaji huyo kutua katika mitaa ya United japo kuwa bosi wa mashetani wekundu Erik Ten Hag anauhitaji mkubwa wa kuidaka saini ya mshambuliaji huyo wa raia wa Denmark .

Klabu ya Atalanta walitumia pauni milioni 15 kumnunua Hojlund kutoka Sturm Graz miezi 11 iliyopita na kufunga mabao tisa katika ligi ya Serie A msimu uliomalizika.

Hadi sasa ada ya uhamisho imekuwa kikwazo tangu kuanza kwa mazungumzo na mahitaji ya Atalanta ya pauni milioni 86 zaidi ya kile ambacho United walikuwa wakitarajia kulipa huku tayari wametumia pauni milioni 110 kufanya usajiliwa Mason Mount na Andre Onana

Kwa mujibu wa habari, United haiko tayari kutumia zaidi ya pauni milioni 60 katika kumsaka mshambuliaji huyo wa Atalanta.Wakati huohuo, Mashetani Wekundu wanaripotiwa kutaka kumnunua nyota wa PSG Kylian Mbappe huku wakihusishwa na Randal Kolo Muani wa Eintracht Frankfurt.

Chanzo: Mwanaspoti