Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Mdenimark Rasmus Hojlund amekuwa mchezaji wa pekee kwa klabu hiyo kufunga magoli manne kwenye mechi 4 mfululizo akiwa na umri wa miaka 21 kushuka chini.
Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Mdenimark Rasmus Hojlund amekuwa mchezaji wa pekee kwa klabu hiyo kufunga magoli manne kwenye mechi 4 mfululizo akiwa na umri wa miaka 21 kushuka chini. Hojlund ameweka rekodi hiyo jana baada ya kufunga goli lake la 4 katika mchezo dhidi ya wagonga nyundo wa London, Westham United katika uwanja wa Old Trafford na kupata ushindi wa magoli 3-0 katika mchezo wa mzunguko wa 23 wa ligi kuu nchini Uingereza EPL