Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hojlund ampigia debe Eriksen

Hojlund X Eriksen Hojlund ampigia debe Eriksen

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Manchester United, Rasmus Hojlund amempigia debe Christian Eriksen ni mchezaji bora na anastahili kupewa nafasi, ikiwa ni siku chache tangu kuibuka kwa taarifa za nyota huyo wa kimataifa wa Denmark hana furaha klabuni hapo.

Taarifa hizo zinaeleza pia kiungo huyo wa zamani wa Tottenham anafikiria kuondoka mwisho wa msimu kutokana na kutokupata nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha Kocha Erik ten Hag.

Kwenye kikosi cha Man United msimu huu, nyota huyo amecheza mechi nane tu za Ligi Kuu England ikiwa ni tofauti na msimu uliopita akicheza mechi nyingi.

Akizungumza na TV2 Hojlund alisema: “Binafsi niliwahi kukaa kwenye benchi nilipokuwa Copenhagen, kiuhalisia kila mchezaji anataka kucheza kila siku, lakini bado ameendelea kucheza vizuri mazoezini na kuonyesha ukomavu, licha ya kukosa nafasi ameonyesha kuwa na furaha kwa hiyo sioni kama kuna shida sana.”

“Alipata nafasi dhidi ya Liverpool na akaonyesha kiwango bora, ni mchezaji mzuri, kila siku ungependa kumwona uwanjani lakini huo unabaki kuwa ni uamuzi wa kocha ikiwa anataka kumchezesha au laa,” alisema Hojlund na kusisitiza yeye anamwona Eriksen kama mmoja wa viungo bora kwenye kikosi chao.

Eriksen hivi karibuni alifunguka haridhishwi na kitendo cha kuwekwa benchi mara kwa mara na ameshazungumza na Erik ten Hag juu ya hilo.

“Nilishasema hapo mwanzo siridhishwi na kutokucheza lakini sio kitu kinachonifanya nikose usingizi, timu inafanya vizuri na natakiwa niheshimu hilo, ninachokifanya ni mazoezi na kujiweka sawa ili niwe tayari kwa mechi yoyote nitakayopangwa. Nimeshazungumza na Ten Hag juu ya hili na kumwambia nahitaji kucheza mechi nyingi kadri inavyowezekana.”

Eriksen ambaye huu ni msimu wake wa pili kwenye kikosi cha mashetani hao wekundu hadi sasa amecheza mechi 65 za michuano yote amefunga mabao matatu na kutoa asisti 12.

Chanzo: Mwanaspoti