Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hojlund akili yake yote ilikuwa Man United

Rasmus Hojlund Miss Hojlund akili yake yote ilikuwa Man United

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Rasmus Hojlund amesema kua vilabu vingi vilikua vinahitaji saini yake lakini yeye alikua anaiwaza Man United tu.

Hojlund alijiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Atalanta ya nchini Italia alikua kipaumbele kwa klabu ya Man United kwenye dirisha kubwa lililopita, Lakini vilevile yeye alikua ameipa klabu hiyo nafasi ya kwanza kama timu anayotaka kujiunga nayo.

Mshambuliaji huyo raia wa kimataifa wa Denmark amefanikiwa kucheza mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo juzi kwenye kipigo dhidi ya klabu ya Arsenal, Hiyo ikitokana na majeraha yaliyokua yanamuandama.

Mshambuliaji huyo amepokea sifa kwa mashabiki wa klabu hiyo kutokana na dakika chache tu alizozicheza katika mchezo wa juzi dhidi ya Arsenal, Huku wakieleza ameonesha hali ya upambanaji wakitarajia makubwa zaidi kutoka kwake.

Rasmus Hojlund licha ya kufunga mabao machache akiwa ndani ya klabu ya Atalanta msimu uliomalizika,Lakini Man United walivutiwa na kiwango chake alichokionesha huku suala la umri pia likiwa kipaumbele wakiamini ana uwezo kuboresha uwezo wake kutokana na umri aliokoa nao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live