Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hofu yatanda Biashara United, yahitaji Sh140 milioni

Biashara Milioni Hofu yatanda Biashara United, yahitaji Sh140 milioni

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Miezi kadhaa baada ya uongozi wa Biashara United kuikabidhi kampuni ya Free Sports kuiendesha timu hiyo kutokana na ukata huku wakikubaliana iwasaidie kulipa madeni, kampuni hiyo imejitoa na kuiacha bila msaada jambo ambalo limezua hofu juu ya hatma ya ushiriki wake kwenye Championship.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 6, 2023 mjini Musoma, Katibu Mtendaji wa Biashara United, Maria Lima amesema hatua hiyo inawaweka kwenye hatihati ya kumaliza msimu kwenye ligi ya Championship kutokana na ukata unaowakabili huku akiomba msaada wa wadau.

Amesema kwa sasa timu hiyo inahitaji zaidi ya Sh140 milioni ili kuweza kushiriki na kumaliza msimu huo, ambapo hali hiyo imetokana na kitendo cha kampuni ya Free Sports kujitoa na kuiacha huku wachezaji wakiwa kambini bila msaada wowote.

"Awali timu ilikuwa ikiendeshwa na wanachama baadaye kampuni ilikabidhiwa kwaajili ya uendeshaji lakini nimepokea taarifa jana asubuhi juu ya kampuni hii kujitoa na hivyo timu kubaki bila msaada wowote na hatuna pa kukimbilia"

"Wakati kampuni inajitoa ikumbukwe kuwa vijana wapo kambini na hivi tunavyoongea hawana hata chakula achilia mbali madai yaliyopo kama mishahara kwa ujumla hali siyo nzuri" amesema Mariam

Katibu huyo amesema kuna athari nyingi zinazoweza kuikabili timu hiyo endapao haitakamilisha michezo iliyobaki ikiwa ni pamoja na kupokwa point 12 kila itakaposhindwa kutokea uwanjani jambo ambalo amesema kuwa asingependa litokee.

“Tupo nafasi ya tisa tukiwa na pointi 24 na tumebakiza michezo mitano kukamilisha msimu kwahiyo nawaomba wana Mara waliopo ndani na nje ya mkoa, wadau wote wa soka na michezo nchini wajitokeze waisaidie timu vijana wana morali kubwa tatizo ni fedha tu," amesema

Naodha wa timu hiyo, Abdallah Mtei amesema kutokana na changamoto zinazowakabili hawajui nini hatma yao hivyo kuwaomba wadau wote waweze kushirikiana na kuiokoa timu hiyo.

"Hii kazi ndiyo inayotupatia kipato na pamoja na changamoto zote vijana bado tuna morali lakini kwa hali ilivyo hatujui tunafanyaje niwaombe wana Mara kwa umoja wao watusaidie kwani timu hii ni fahari ya mkoa," amesema

Chanzo: Mwanaspoti