Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi timu zimeshinda mara nyingi dakika za majeruhi EPL

Darwin Nunez3 1200x630 Darwin Nunez

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu England mara zote imekuwa maarufu kwa mabao ya dakika za majeruhi.

Unakumbuka lile bao la Sergio Aguero la dakika 94 lililoipa ubingwa wa kwanza Manchester City kwenye Ligi Kuu England mwaka 2012? Asikwambie mtu, mabao ya ushindi ya dakika za majeruhi yana raha yake.

Manchester United ilijipatia umaarufu wa mabao ya aina hiyo enzi za kocha Sir Alex Ferguson na kipindi hicho yalifahamika kama ‘Fergie Time’. Mechi za Man United zilikuwa hazijaisha hadi ziishe kabisa.

Jumamosi iliyopita, Man United ilihitaji kufunga mara mbili kupitia kwa kiungo wake Scott McTominay kwenye dakika za majeruhi ili kuichapa Burnley 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Hata hivyo, unajua timu inayoongoza kwa kufunga mabao ya ushindi mara nyingi kwenye dakika za majeruhi? Kwa mujibu wa Opta, hizi hapa timu zilizopata ushindi mara nyingi kwa kufunga mabao ya ushindi dakika za majeruhi kwenye Ligi Kuu England.

9.Aston Villa - 17

Kuanzia nafasi ya tisa ni klabu iliyo na wazawa wengi ambao wamefurahia ushindi wa dakika ya 90 mara 17 katika historia ya klabu yao. Katika mechi ya mechi ya hivi karibuni dhidi ya Crystal Palace, vijana wa Unai Emery walitoka nyuma kwa bao 1-0 dakika ya 87 na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Idadi ya ushindi wa dakika za majeruhi ingekuwa kubwa zaidi, endapo isingeshuka daraja kati ya mwaka 2016 na 2019.

8.Man City - 18

Bao la Sergio Aguero la dakika ya 90 dhidi ya Queens Park Rangers linakumbukwa zaidi katika historia ya Ligi Kuu England. Huu ni ushindi bora zaidi kutokea kwa Man City mwaka 2012. Hata hivyo, kutokana na klabu hiyo kutoshiriki Ligi Kuu England mara kwa mara tangu kuanzishwa bila shaka idadi itapungua kidogo.

Waliwahi kupata ushindi dakika ya 97 kutokana na bao la Raheem Sterling dhidi ya Bournemouth mwaka 2017, pamoja na bao la Kelechi Iheanacho dhidi ya Crystal Palace miaka miwili iliyopita, ambalo lilikuwa bao lake la kwanza kwa klabu hiyo.

7.Newcastle United - 21

Newcastle ilikuwa na nyakati nzuri miezi ya hivi karibuni ukijumuisha na bao alilofunga Bruno Guimaraes dakika ya 95 dhidi ya Leicester City mwisho wa msimu wa 2021-2022. Ushindi mwingine waliopata wa dakika za majeruhi ulikuwa mwaka 2020 walipocheza nyumbani dhidi ya Chelsea. Bao jingine la kukumbukwa la dakika za lala salama lilikuwa dhidi ya Arsenal katika mechi iliyomalizika kwa sare ya mabao 4-4.

6.Everton - 24

Everton imekuwa na matukio ya kushangaza kwa miaka mingi, moja ya matukio muhimu zaidi miaka ya hivi karibuni ilikuwa dhidi ya Newcastle mwaka 2022. Everton ilikuwa ikipambana kuepuka kushuka daraja lakini bao la dakika ya 97 dhidi ya Newcastle liliwabeba na kunusurika kushuka kutoka Ligi Kuu England.

Pia Everton ilipata ushindi wa mabao 2-1 wa dakika za majeruhi dhidi ya Arsenal mwaka 2002, shukrani kwa bao la jioni la Wayne Rooney alipofunga bao lake la kwanza akiwa na umri wa miaka 16 na kuhitimisha mwendo mbaya wa timu hiyo wa kucheza mechi 30 bila ya kupata ushindi dhidi ya washika mitutu hao wa London.

Rooney haku-ishia hapo alifunga bao la kushangaza dhidi ya Aston Villa mwaka 2003 alipokuwa na umri wa miaka 17.

5.Chelsea - 26

Chelsea ina rekodi nzuri ya kushinda dakika za majeruhi. Jorginho alifunga bao dakika 90 kwa mkwaju wa penalti dhidi ya Leeds United na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Samford Bridge mwaka 2021. Ushindi mwingine wa dakika za majeruhi ulikuwa dhidi ya Stoke City mwaka 2000, Florent Malouda alipofunga zikiwa zimebaki dakika tano mwisho wakanyakua ubingwa wa Ligi Kuu England.

4.Man United - 27

Ikizingatiwa kuwa Manchester United ilijitengenezea sifa ya kushinda mechi mfululizo katika dakika za mwisho chini ya Sir Alex Ferguson, labda ni jambo la kushangaza haiongozi katika orodha au hata kuingia tatu bora. Pamoja na hayo, bado ina idadi ya mabao ya dakika ya 90, hasa ukizingatia Marcus Rashford alifunga mabao manne ya dakika za majeruhi - zaidi ya mchezaji mwingine yeyote ambaye ameweza kufunga katika historia ya Ligi Kuu England. Wikiendi iliyopita Man United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dakika za majeruhi dhidi ya Brentford zikiwa zimeongezwa dakika sita za nyongeza. Mashetani Wekundu walikuwa nyuma kwa bao moja kabla ya Scott Mctominay kupachika mabao mawili.

3. Tottenham Hotspur - 30

Ingawa ni timu ambayo inapondwa na mashabiki kwa sababu haijawahi kubeba medali katika historia ya klabu hiyo, lakini Spurs ina historia nzuri ya kupata ushindi katika dakika za majeruhi. Mfano mzuri ni mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Sheffield United. Spurs ilipambana na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dakika za lala salama. Richarlison alisawazisha katika dakika ya 98 kabla ya Dejan Kulusevski kufunga bao la ushindi katika dakika ya 100.

2. Arsenal - 31

Arsenal imeshinda mechi dakika za majeruhi zaidi ya Spurs, na msimu huu tumeshuhudia dhidi ya Manchester United ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1. Declan Rice alifunga katika dakika za lala salama matokeo yakiwa 2-1 kabla ya Gabriel Jesus kufunga bao la ushindi kwenye Uwanja wa Emirates. Msimu uliopita tulishuhudia bao la dakika za majeruhi dhidi ya Bournemouth katika ushindi wa mabao 3-2.

1. Liverpool - 42

Mwisho, Liverpool ndio inatufungia ukurasa katika orodha hii kwani ndio inaongoza kwa kufunga mabao dakika za majeruhi zaidi ya timu nyingine. Mfano mechi dhidi ya Man United waliyoshinda nyumbani dakika ya 98 Liverpool ikiibuka na ushindi wa mabao 7-0 bila kusahau walipoichakaza pia Norwich City. Hivi karibuni Liverpool ilishinda mechi dakika za majeruhi dhidi ya Newcastle baada ya Darwin Nunez kuingia akitokea benchi na kuisawazishia timu yake na kufunga bao la ushindi.

Chanzo: Mwanaspoti