Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi sura haziuzwi Man United

Onanaaaaaa Hizi sura haziuzwi Man United

Fri, 31 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Habari ndo hiyo. Manchester United imeripotiwa haitachekelea ofa yoyote ya kumhusu kipa wao Andre Onana kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, wakiwa na maana Mcamerooni huyo, hauzwi.

Kinachoonekana kipa Onana amewekwa kwenye kundi la wachezaji wasioguswa katika kikosi hicho, kwa mantiki hata iweje, hawatauzwa.

Onana, 28, aliwasili Old Trafford kwa ada ya Pauni 47.1 milioni akitokea Inter Milan mwaka jana. Alianza maisha yake huko Old Trafford kwa ugumu mkubwa Ligi Kuu England baada ya kufanya makosa kadhaa uwanjani.

Lakini, baadaye kipa huyo alitulizana vyema golini na sasa Man United imefichua itabaki na huduma ya kipa wao huyo namba moja iwe Erik ten Hag ataondoka au atabaki. Mmiliki wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe amepanga kufanya maboresha makubwa kwenye kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, ili mambo kwenda sawa, Man United italazimika kuuza baadhi ya wachezaji.

Awali Man United ilitoa orodha ya wachezaji watatu ambao hata iwe vipi hawauzwi na sasa imemwongeza Onana na kufanya kuwa wanne na hata uweke ofa kiasi gani mezani, hawauzwi.

Wachezaji hao watatu wa awali ni makinda, Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho na Rasmus Hojlund. Garnacho na Mainoo waliibukia kwenye akademia ya Man United, wakati Hojlund alinaswa kwa ada ya Pauni 72 milioni kutokea Atalanta dirisha la uhamisho la mwaka jana.

Imeelezwa wengine wote wanauzwa kama ofa itakayowekwa mezani inashawishi. Kwenye hilo hata nahodha, Bruno Fernandes anauzwa, licha ya Mreno huyo kudai amekuwa na furaha kwa kuendelea kukipiga Old Trafford.

Wachezaji Antony, Mason Greenwood, Aaron Wan-Bissaka, Christian Eriksen, Casemiro na Donny van de Beek nao wanaweza kuondoka baada ya Wafaransa wawili, Anthony Martial na Raphael Varane kuthibitika wanaondoka.Complex

Chanzo: Mwanaspoti