Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndo fowadi za mastaa watatu balaa kwa mabao 2021/22

Foward Pic Data Nyota wa Kikosi cha PSG

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Masupastaa Lionel Messi, Kylian Mbappe na Neymar ilionekana kama kombinesheni yao ingekuwa shida kubwa kwa makipa huko Ulaya baada ya mafowadi hao watatu kuwapo kwenye kikosi kimoja cha Paris Saint-Germain.

Baada ya PSG kumsajili Messi kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka jana, mashabiki wa soka duniani walishtuka na kuwaonea huruma makipa ambao wangekutana na miamba hiyo ya Ufaransa kutokana na tayari kuwa na washambuliaji moto, Neymar na Mbappe kwenye kikosi chao kabla ya kuongezeka kwa Muargentina huyo.

Hata hivyo, mambo yamekuwa si mambo. Kombinesheni ya Messi-Mbappe-Neymar imeshindwa kutiki, PSG ikiishia kubeba Ligue 1 tu, ikitupwa nje ya Coupe de France na kuondoshwa kwenye hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Messi ni kama amepoteza buti zake za kufunga mabao tangu alipotua Parc des Princes akitokea Camp Nou. Hata hivyo, kwa mujibu wa takwimu za Transfermarkt, safu hiyo ya ushambuliaji imefunga mabao mengi kwelikweli kwa msimu wa 2021/22 kwa maana ya kuweka pamoja mechi za ligi, makombe ya ndani, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League.

Kutokana na hilo, hizi hapa safu za washambuliaji watatu zilizofunga mabao mengi zaidi kwa msimu wa 2021/22 kwa mikikimikiki ya Ligi Kuu.

21. Atalanta mabao 41

Mario Pasalic (14), Luis Muriel (14) and Duvan Zapata (13)

20. Marseille mabao 41

Arkadiusz Milik (16), Dimitri Payet (13) and Cengiz ‹nder (12)

19. Sassuolo mabao 41

Gianluca Scamacca (16), Domenico Berardi (15) and Giacomo Raspadori (10)

18. Leicester City mabao 42

Jamie Vardy (17), James Maddison (15) and Patson Daka (10)

17. West Ham United mabao 42

Jarrod Bowen (18), Michail Antonio (13) and Said Benrahma (11)

16. Napoli mabao 44

Victor Osimhen (18), Lorenzo Insigne (13) and Dries Mertens (13)

15. Stade Rennais mabao 44

Martin Terrier (21), GaÎtan Laborde (12) and Benjamin Bourigeaud (11)

14.Tottenham Hotspur mabao 49

Heung-min Son (23), Harry Kane (21) and Dejan Kulusevski (5)

13. Real Betis mabao 50

Juanmi (20), Borja Iglesias (19) and Willian Jose (11)

12. Borussia Dortmund mabao 51

Erling Haaland (29), Marco Reus (13) and Donyell Malen (9)

11. Bayer Leve rkusen mabao 51

Patrik Schick (24), Moussa Diaby (17) and Florian Wirtz (10)

10. Lyon mabao 51

Moussa Dembele (22), Karl Toko Ekambi (18) and Lucas Paqueta (11)

9. Inter Milan mabao 52

Lautaro Martinez (25), Edin Dzeko (17) and Ivan Perisic (10)

8.Lazio mabao 53

Ciro Immobile (32), Sergej Milinkovic-Savic (11) and Pedro (10)

7.AS Monaco mabao 56

Wissam Ben Yedder (32), Kevin Volland (15) and Sofiane Diop (9)

6. Manchester City mabao 60

Riyad Mahrez (23), Kevin De Bruyne (19) and Raheem Sterling (17)

5.Paris Saint-Germain mabao 63

Kylian Mbappe (39), Neymar (13) and Lionel Messi (11)

4.RB Leipzig mabao 63

Christopher Nkunku (35), Andre Silva (17) and Emil Forsberg (11)

3.Liverpool mabao 75

Mohamed Salah (31), Sadio Mane (23) and Diogo Jota (21)

2.Real Madrid mabao 77

Karim Benzema (44), Vinicius Junior (21) and Marco Asensio (12)

1. Bayern Munich mabao 81

Robert Lewandowski (50), Serge Gnabry (17) and Leroy Sane (14)

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz