Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndizo timu zilizopigwa tano tano na Yanga msimu huu

Yanga Tano Tano Ms Hizi ndizo timu zilizopigwa tano tano na Yanga msimu huu

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya Yanga imekuwa timu ya kwanza nchini Tanzania kushinda magoli (5) katika kila mashindano inayoshiriki ndani ya msimu mmoja.

Baada ya kuifunga bao 5-0 Klabu ya soka ya Ihefu hapo jana katika Dimba la Chamazi na kulipa kisasi, Yanga imefikisha timu 8 ambazo imezifunga mabao 5 msimu huu wakiwemo watani zao Simba SC.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi anatajwa kuwa ndiye kocha katili zaidi kuwahi kutokea kwenye Klabu ya Yanga SC, na amedhihirisha hilo kwa vitendo kwani timu yake hata kama ikifunga mabao mengi, hapaki basi kulinda ushindi badala yake anaongeza nguvu zaidi kusaka mabao mpaka kipenga cha mwisho.

Timu ambazo zimeshakula chuma tano tano mpaka sasa kutoka kwa Wananchi wa mitaa ya Twiga na Jangwani ni hizi;

◉ Yanga 5 - 0 KMC - NBCPL

◉ Yanga 5 - 0 JKT Tanzania - NBCPL

◉ Yanga 5 - 1 ASAS - CAF CL

◉ Yanga 5 - 1 Simba SC - NBCPL

◉ Yanga 5 - 0 Jamhuri - Mapinduzi Cup

◉ Yanga 5 - 1 Hausing Fc - ASFC

◉ Yanga 5 - 0 Polisi Tanzania - ASFC

◉ Yanga 5 - 0 Ihefu FC - NBCPL

Iko hivi, Tanzania hakuna timu yenye uwezo wa kupishana na Yanga kwa sasa, timu zote zilizoleta kiburi na kukosa heshima msimu huu zimepigwa kama ngoma.

Timu zingine zilizojaribu kuleta kiburi ziliadhibiwa pia, baadhi yao;

◉ Yanga 4 - 0 CR Belouizdad - CAFCL

◉ Yanga 3 - 0 Medeama - CAFCL

◉ Yanga 2 - 0 Azam FC - Ngao ya Jamii

◉ Yanga 3 - 2 Azam FC - NBCPL

◉ Yanga 2 - 0 Singida FG - NBCPL

◉ Yanga 4 - 1 Mtibwa Sugar - NBCPL

◉ Yanga 3 - 0 KMC - NBCPL

◉ Yanga 3 - 0 Geita Gold - NBCPL

Mpaka sasa hakuna timu iliyomzidi Yanga kwa umiliki wa mpira katika timu zote alizocheza nazo Tanzania.

Nini maana yake?

Timu zilizokubali kuwa watumwa, kuwa hazina uwezo wa kupishana na Yanga zikapaki basi watu (10) golini ndizo zilizopata kipigo kidogo.

◉ 1 - 0 Namungo FC

◉ 2 - 1 Mashujaa FC

◉ 1 - 0 Dodoma Jiji

◉ 0 - 0 Kagera Sugar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live