Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndizo rekodi zilizowekwa na Timu ya Morocco Kombe la Dunia

Morocco 1 Erf Morocco wametinga hatua ya Robo Fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya Taifa lao

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Morocco imepeperusha vyema bendera ya bara la Afrika dhidi ya Hispania baada ya kuindosha kwa mikwaju ya penalti 3-0 kwenye raundi ya 16 bora katika Fainali za Kombe la Dunia 2022 na kuweka rekodi mbili.

Mchezo huo ulimalizika kwa dakika 90+30 za nyonyeza bila ya kucheka na nyavu kwa pande zote mbili na kulazimisha kuingia hatua ya matuta yaliyoipeleika Hispania nyumbani.

Hispania ilishindwa kupata penalti hata moja kupitia wachezaji wao Pablo Sarabia, Sergio Busquets na Carlos Soler huku kipa wa Morocco, Yassine Bounou akiibuka kinara baada ya kupangua penalti mbili na moja ikigonga mwamba.

Mastaa Sabiri, Hakim Ziyech na nyota wa Paris Saint-Germain, Achraf Hakimi walimtungua kipa Unai Simon na kuipa Morocco ushindi kwa penalti 3-0 huku taifa hilo likiweka rekodi mbili kwenye michuano hiyo.

Sasa Morocco imeweka rekodi ya kuwa nchi ya nne kutoka Afrika kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia 2022, Qatar. Vile vile inakua timu ya kwanza bara la Afrika ambayo haijaruhusu bao katika mechi za hatua ya makundi.

Vilevile Morocco inakuwa timu ya nne kutoka Afrika kutinga hatua ya robo fainali katika historia ya Kombe la Dunia ikitanguliwa na Cameroon (1990) Senegal (2002), na Ghana (2010).

Morocco itachuana na Ureno kwenye mtanange wa robo Fainali ya Kombe la Dunia 2022. Wakati huo huo mkongwe wa Cameroon na Rais wa Shirikisho la soka la taifa hilo Samuel Eto'o, akitoa pongezi baada ya Morocco kufuzu ikiibuka na ushindi huo dhidi ya Hispania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live