Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndizo dabi 10 kubwa Uingereza

Haaland Vs United Hizi ndizo dabi 10 kubwa Uingereza

Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Neno derby halina tafsiri yake kwa sababu limeazishwa huko bara la America ya Kusini lakini baadae lilipewa maana yake ambayo kwa Kiswahili tunasema (MAHASIMU) watu ambao wameshashindwa kuelewana kutokana na sababu zikiwemo usaliti na Chuki za wazi wazi.

Kiufupi derby inahusisha timu mbili Zenye uhasimu mkubwa wa Eneo mtaa kataa Wilaya mkoa au Jiji au kitaifa mfano Dabi ya nchi ya England ni Watoto wa Mjini kutoka Jiji la Biashara la Liverpool dhidi ya Wana mipango kutoka Jiji lilijitenga la Manchester Manchester United Maarufu kama the Res Devil Dabi ya nchini Tanzania ni Young African's dhidi ya Simba Sc kwa sababu Simba Sc waliwasaliti Yanga na kuanzisha kikundi Chao wakaenda kucheza Ligi ya kulipwa wakikimbia Ligi ya Bure ya wazawa kitu Ambacho kiliwaumiza Yanga kwani wao walikua wakipambania uhuru wa Tanzania Kupitia mpira.

Derby ya Nchi ya Spain ni kati ya Fc Barcelona klabu ambayo ilianzishwa na Dini na Real Madrid klabu ambayo ilianzishwa na familia ya kifalme.

LEO NAKUPA DABI BORA ZA MJI MMOJA ZA NCHINI ENGLAND

01-CELTIC V RANGERS

Hii Ndiyo dabi namba Moja nchini England kumbuka England inajengwa na Nchi zipatazo nne Zenye makao makuu yake London ambapo ndoo Mji mkuu. Vile vile Celtic na Rangers inashika Nafasi ya 02 dabi Bora Duniani ipo Nchini Scotland.

02- EVERTON V LIVERPOOL FC

Hawa wote wanapatikana Jiji Moja la Liverpool chanzo Cha ugomvi wao ni kwamba liver waliwasaliti Everton wakaenda kuanzisha klabu yao nyingine kitu Ambacho kiliwaudhi Mashabiki wa Everton na Uwanjani wa Liverpool na Everton upo umbali wa Mita 900 tu haina haja ya usafiri ni kwa miguu unakanyagia.

Everton hua wapo tayari kufungwa na Manchester United ambaye Ndiye hasimu wa Liverpool ila sio Liverpool na hua wanawauzia wachezaji Manchester United ili wakapambane na liver hata Ubingwa ambao Liverpool ameskosa kwa misimu kadhaa ni sababu ya hao hao msimu huu wamemfunga na ule msimu Manchester City anachukua kwa alama 01 Everton ndoo walitibua kwa kumlazimisha Liverpool sare ya 1-1.

03- ARSENAL vs Tottenham Hotspur

Dabi ya Jiji Moja la London Chanzo cha uhasimu wao ni kwamba Arsenal walikua wakishinda kombe la Ligi wanapita Mitaa ya Spurs wakipiga vijembe kitu Ambacho kilikua kinawaumiza Mashabiki wa Spurs mpaka leo hata kama Arsenal atamfunga Spurs ila kama Kuna timu wanakimbizana kwenye Ubingwa Tottenham hua anapoteza mechi makusudi ili Arsenal wakose kombe kama msimu uliopita.

Mashabiki baada ya kufungwa Magoli matano na Arsenal kwenye mechi ya mzunguko wa Pili Fans waliiandikia Barua timu yao ya Tottenham Hotspur kua wanaomba kupoteza makusudi mbele ya Manchester City kwani wao hawataki Arsenal wachukue Ligi na kweli walifungwa na City.

Halafu Mashabiki hao baada ya kufungwa waliwauliza Mashabiki wa Arsenal kwamba mlitaka tumfunge City kwamba sisi ni ndugu, undugu gani wa kutufunga mabao matano.

Na Kumbuka ARSENAL Ndiyo klabu kubwa na yenye makombe Mengi Jiji Zima la London kitaifa wakishika Nafasi ya 03 nyuma ya Liverpool man utd Wana makombe 36

04- Aston Villa vs Birmingham City

05-Newcastle United vs Sunderland.

06 MANCHESTER CITY vs MANCHESTER UNITED

Hii Dabi haikuwepo sana kwenye orodha ya dabi hatari England kwa sababu Manchester United walikua ni watawala wa Jiji zima walikua na Mashabiki Nyumba kwa Nyumba mtaa kwa mtaa na ndiyo klabu yenye Mashabiki wengi Duniani wakishika Nafasi ya kwanza nafasi ya Pili Fc Barcelona Nafasi ya tatu Fc Bayern Munich nafasi ya Nne Liverpool Chelsea na Real Madrid.

Hii Dabi inaitwa Manchester derby ilianza kupamba moto mwaka 2008 hawana uhasimu mkubwa Sana lakini Manchester City hua anatamani mafanikio ya United ya kua na utawala wa Jiji kitu Ambacho ni kigumu.

07- Sheffield United vs Sheffield Wednesday

08- Millwall vs West Ham United

09- Cardiff City vs Swansea City

10- Portsmouth vs Southampton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live