Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi ndio mechi kali usizopaswa kuzikosa Qatar 2022

Mane Vvd.jpeg Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza litachezwa Qatar

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi hizi zitajumuisha mastaa wa soka wakionyeshana umwamba katika historia ya fainali hizi zitakazofanyika kwa mara ya kwanza Qatar. Hii ni orodha ya mechi kali ambazo hupaswi kuzikosa kuelekea fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kutikisa nyasi mwezi ujao.

Senegal v Uholanzi - Novemba 21

Timu zitakutana katika ufunguzi wa fanaili za Kombe la Dunia mwaka huu, mechi hii inawakutanisha mastaa wawili Sadio Mane na Virgil van Dijl waliowahi kukipiga pamoja Liverpool kabla ya Mane kujiunga na Bayern Munich mwaka huu.

Hii mechi itakuwa na upinzani mkali kutokana na ubora wao. Senegal inacheza fainali hizi ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kubeba ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (Afcon). Senegal itakuwa na matumaini ya kurudia walichokifanya fainali za Kombe Dunia zilizofanyika mwaka 2002 baada ya kuichapa Ufaransa waliokuwa mabingwa watetezi bao 1-0.

Brazil v Serbia- Novemba 24

Brazil inayopewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa fainali za Kombe la Dunia, Qatar kutokana na ubora wa kikosi chao kwani kimesheheni wachezaji wengi wenye vipaji vya kucheza mpira. Kwa upande wa Serbia sio timu ya kubeza, hivyo Brazil itatakiwa kujipanga dhidi yao ili kupata ushindi.Brazil ina matumaini ya kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza baada ya kutobeba kwa muda mrefu.

Hispania v Ujerumani- Novemba 27

Hii ni mechi ambayo si ya kukosa kuelekea fainali za Kombe la Dunia. Mechi hii mejirudia kwani Hispania ina kumbukumbu nzuri ya kuichapa Ujerumani bao 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2008.

Kabla ya kukutana tena mwaka 2008 kwenye nusu fainali ya Euro. mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa mwaka 2020, Hispania ilipoichapa Ujerumani mabao 6-0 kwenye Michuano ya Nations League. Hii itakuwa ni mechi ya kisasi kwa upande wa Ujerumani dhidi ya Hispania. Miamba hii itakutana kwa mara ya nne katika michuano tofauti.

Ureno v Uruguay - Novemba 28

Mechi hii itawakutanisha wakongwe wawili, Cristiano Ronaldo na Edinson Cavani, waliowahi kucheza pamoja msimu uliopita pale Man United. Cavani ametimkia La Liga na anakipiga Valencia kwa sasa. Hii itakuwa mechi ya kuvutia na ushindani kati ya mastaa hao. Fainali hizi huenda zikawa za mwisho kwa mastaa hawa kutokana na umri kuwatupa mkono

Wales v England - Novemba 29

Baada ya Wales kupata tiketi ya kushiriki fainali za mwisho baada ya kucheza mechi yao mwisho ya kufuzu sasa wanatakutana na wapinzani wao England ambao ni taifa moja. Wales inashiriki fainali hizi kwa mara ya kwanza tangu iliposhiriki fainali zilizofanyika mwaka 1958. Nao vijana wa Gareth Southgate wanaamini watatoboa na kufanya vizuri baada ya kuboronga fainali za Euro (2020) zilizofanyika mwaka jana.

Poland v Argentina - Novemba 30

Pengine unaweza kudhani si mechi kubwa ya kutizama. Lakini mechi hii inawakutanisha wakali wawili wa kufumania nyavu Robert Lewandowski anayeiwakilisha Poland and na Lionel Messi akiiwakilisha Argentina. Wawili hawa wamefunga jumla ya mabao 1,189 ngazi ya klabu yakijumuishwa pamoja. Kila mmoja amepata mafanikio ya kubeba tuzo mbalimbali miaka ya hivi karibuni. Lewandowski alimpiku Messi FIFA ilipomtunuku Tuzo ya Mchezaji Bora wakati Messi akibeba Tuzo ya Ballon d’Or mwaka jana.

France v Australia - Novemba 22

Hii ni mechi ya marudio kwani timu hizi zilikutana katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 2018. Ufaransa na Australia zilikutana katika ufunguzi wa fainali hizo zilizofanyika Russia. Ufaransa inatinga Qatar ikiwa na presha ya kulibeba kwa mara ya pili kama ilivyotokea kwa Brazil mwaka 1958 na 1962.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live