Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hizi hapa takwimu zote za Yanga dhidi ya Bamako

Yanga Sare Mali.jpeg Hizi hapa takwimu zote za Yanga dhidi ya Bamako

Mon, 27 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga wameendelea kuweka hai matumaini yao ya kutinga hatua ya robo fainali kufuatia kukusanya pointi moja wakiwa ugenini.

Bao la Fiston Mayele dakika ya 60, lilitosha kuwapa uongozi vijana wa Nasreddine Nabi kabla ya wenyeji, Real Bamako kuchomoa kwa Kona dakika za nyongeza kupitia kwa Kone.

Yanga ilianza vibaya kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi Monastir kabla ya kuitandika TP Mazembe kwa Mkapa kwa mabao 3-1 na sasa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Bamako.

Hizi ni dondoo muhimu kuhusiana na mchezo huo ambao umeifanya Yanga kufikisha pointi nne, nyuma kwa pointi tatu ambazo wameachwa na vinara wa kundi D, Monastir yenye pointi saba.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga ilipiga mashuti manne huku shuti moja kati ya hayo likilenga lango la Real Bamako ya Mali.

Djigui Diarra ambaye aliokoa hatari tatu ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza alikuwa akikabiliana na ndugu zake wa Mali kwenye mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Jumla ya faulo 18 zilichezwa katika kipindi cha kwanza, Yanga iliongoza kwa kufanya madhabi mara 11 huku Real Bamako mara saba na waliadhibiwa kwa mchezaji wao mmoja, Ibourahima Sidibe kuonyeshwa kadi ya njano.

Dakika ya 40, Yanga iliwalazimu kufanya mabadiliko ya lazima, baada ya Khalid Aucho kuumia na nafasi yake kuingia Aziz Ki.

Huu ni mchezo wa kwanza msimu huu kwa Yanga kwenda mapunziko matokeo yakiwa suluhu kwenye michano ya Kimataifa, dhidi ya Monastir walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 na TP Mazembe wakawa mbele kwa mabao 2-0.

Bao alilofunga Fiston Mayele dakika ya 60 kwenye uwanja wa 26 Mars, lilikuwa la nne msimu huu kwa Yanga kwenye Kombe la Shirikisho Afrika huku likiwa la kwanza kwa mshambuliaji huyo kwenye hatua ya makundi.

Kati ya mashuti mawili ambayo Yanga ilipiga ndani ya dakika 10 za kipindi cha pili yalipigwa na Mayele huku moja kati ya hayo ikiwa bao.

Ndani ya dakika 90 za mchezo huo, Yanga ilipiga pasi 431 kwa Real Bamako wakipiga 346, Wananchi walikuwa na usahihi wa pasi zao kwa asilimia tatu zaidi ya Wamali. Yanga 73, Bamako 70.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live